YAANI UNAAMBIWA PATI YA BETHIDEI YA MSANII BABY MADAHA UCHAFU 85%..JIONEE MWENYEWE HAPAA

Admin Updates11 years ago102 Views

Stori: Issa Mnally SHEREHE
ya siku ya kuzaliwa ya msanii wa muziki na filamu, Baby Joseph Madaha
‘Baby Madaha’ iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Kijitonyama
jijini Dar es Salaam, ilitawaliwa na vitendo vichafu mwanzo mwisho.


Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’akiogeshwa pombe na mashosti zake.


Hafla hiyo iliyohudhuriwa na watu wachache wakiwemo baadhi ya
wasanii, ilifanyika katika Grosari moja iliyopo Kijitonyama.Miongoni mwa
mastaa waliohudhuria alikuwa ni mcheza soka wa zamani wa timu ya Yanga
ya jijini Dar, Samson  Mwamanda.


Sherehe hiyo iliyoanza mishale ya saa 6.00 usiku ilitawaliwa na
vituko kibao vilivyowaacha midomo wazi baadhi ya wahudhuriaji.Moja ya
vituko hivyo ni pale Baby Madaha aliyekuwa amekolea kwa kilevi alipoamua
kupigana denda laivu na msanii Isabela Mpanda ambaye naye alikuwa
kachangamka ile mbaya.


 
Baby Madaha akifurahia bethidei na shosti yake Isabela.


Isabela alikuwa kituko zaidi kufuatia kuvaa kinguo kifupi cha pinki
kilichoacha sehemu kubwa ya mwili wake, hasa kuanzia mapajani kuwa wazi.


Msanii huyo pamoja na kujitupa huku na huko kilevi na kucheza muziki
kwa kukata nyonga kinoma, alikuwa akiinua nguo yake juu na kuonesha
kufuli lake ‘white’ na kujishika sehemu za nyuma jambo lililomfanya
mmoja wa wahudhuriaji kusema:


 
Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’akiwa amelowa pombe.


“Jamani pombe ni noma, mnaona mambo ya aibu anayoyafanya Isabela?”
Kituko kingine ni pale mastaa hao waliokuwa bwii kwa kilevi akiwemo
Mwamanda, walipoamua kummwagia pombe kichwani na kwenye nguo zake Baby
Madaha baada ya kumuimbia wimbo wa ‘Happy birth day to you…!’

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.