Uchaguzi Mkuu 2025:Dkt Joel Nanauka achukua fomu jimbo la Mtwara Mjini kuupitia CCM.

Masama BlogKITAIFAMATUKIOSIASA5 months ago429 Views

Mwana maudhui,mtaalamu ba mbobezi wa kuelimisha jamii Dkt.Joel Arthur Nanauka mzaliwa wa Mtwara amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama cha mapinduzi jambo la mtwara mjini ambapo amesema zoezi hilo limeenda vyema na ana imani kubw akuelekea mchakato wa uteuzi wa wagombea.

Akiongea baada ya kuchukua fomu mapema ofisi ,a CCM zilizopo mjini mtwara kwenye jengo la CCM mkoa wa Mtwara Nanauka ameonyesha kuridhishwa na jinsi Chama Cha Mapinduzi kilivyojipanga kuhakikisha zoezi hilo linakuwa kama mazoezi ya miakka mingine ambapo mwaka huu CCM hairuhusu mbwembwe wala shamrashamra za wapambe wakati wa kuchukua fomu.

Joel Nanauka ni mtaalamu wa masuala ya maendeleo na diplomasia ya uchumi ambaye anajishughulisha zaidi na prorgam za kuboresha maisha ya watu.

Ni mkurugenzi wa taasisi ya Nanauka Foundation inayoendesha programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi, kiafya na misaada ya kielimu kwenye maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Amejikita katika kutoa mafunzo kwenye eneo la maendeleo binafsi (Personal Develoment) na amewahi kutajwa katika orodha ya vijana 100 barani Afrika wenye mchango chanya kwa jamii yao. Pia mwaka 2024 alitajwa katika orodha ya watanzania 100 waliotoa mchango chanya nchini.

Ni mkufunzi katika mashirika na makampuni mbalimbali ndani na nje ya nchi. Mhitimu wa shahada ya Uongozi na Biashara, Stashahada ya juu ya Diplomasia ya Uchumi, Shahada ya Uzamili katika Maendeleo na Uhusiano wa kimataifa, Shahada ya Uzamili ya Uongozi na Shahada ya heshima ya Uzamivu.

Amewahi kuwa mwajiriwa wa Umoja wa Mataifa kabla hajaanzisha taasisi yake ya Africa Success Academy inayojikita kujenga rasilimali watu ndani na nje ya Nchi. Dkt.Joel Nanauka ni msomi na mbobezi ambapo katika historia yake aliwahi kuwa mwanafunzi bora kifaifa(Tanzania one) alipohitimu masomo ya Sekondari.

Aidha Nanauka amewahi kuandika vitabu 9 tofauti vyenye lengo la kuelimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ya kiuchumi na kimaendeleo Kikiwepo kitabu chake Maarufu cha Timiza Malengo Yako.

Masama Blog Tunamtakia kila la Heri Dkt Nanauka katika safari yake hii ya kisiasa kuelekea vikao vy auteuzia vya Chama Cham mapinduzi.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...