

“Hakuna
sehemu ambayo ungemkuta Romy bila mimi kuwepo. Yalikuwa ni maisha f’lani
ambayo natamani yajirudie. “Ukweli Romy alikuwa ni mkubwa kwangu lakini
tuliishi kama mapacha licha ya kwamba Romy alikuwa mtundu kuliko mimi.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Ishu ya shule ikawaje?
Kwa namna tulivyokuwa ilikuwa ngumu kupelekwa shule tofauti, tulisoma shule moja kuanzia shule ya msingi hadi sekondari.
Ubishoo ilikuwa
tangu utotoni
“Unajua
sisi wazazi wetu walikuwa wa kisasa, walikuwa wanajua kutuvalisha
vizuri na ndiyo maana picha nyingi za utotoni cheni, raba, jinzi na
tisheti za kijanja kama kawa. Kwa hiyo huu usafi hatukuuanzia juzi wala
jana, sisi tangu ‘long time’ kitambo.”
Walichopendelea zaidi
“Enzi
hizo tukiwa wadogo hatukujua kama tutakuja kufanya muziki, tulifanya
mambo mengi ya kitoto tu. Tulikuwa tunacheza sana mpira kama ilivyo kwa
watoto wengine.”
Muziki ilikuwaje?
“Wakati tuko wadogo,
nakumbuka kuanzia tukiwa shule ya msingi, mama yangu alikuwa akitupeleka
sana kwenye maeneo ya burudani. Ikitokea kuna mashindano ya kuimba
‘talent show’ alikuwa akitushika mkono na kutupeleka, huko ndiko
tulikoanzia mambo ya muziki.”
Mwanzo wa ustaa
Romy
alipokuwa akifanyiwa ‘intaviu’ katika Kipindi cha Sporah hivi karibuni
alisema: “ Wakati nilipoanza kufanya kazi ya utangazaji pale Clouds,
Diamond hakuwa lolote, alikuwa akiniona kwenye TV, yeye bado anapambana
na maisha ya uswahilini huku akifanya muziki.
“Wakati mimi naanza kupata zile elfu 10 na zaidi, yeye alikuwa hana hata mia. Nikawa namtoa kimtindo.
“Ikafika
kipindi ndiyo nikamtambulisha Diamond kwa watangazaji wenzangu akiwemo
Adam Mchomvu, nikawaambia nina mdogo wangu anaitwa Diamond anaimba,
tunamsaidiaje.
“Tukarekodi nyimbo kibao zikaishia hewani. Kuna
moja ya kurap tukafanya na Gez Mabovu na Gwea (wote marehemu) kisha
nikaipeleka Clouds. Mchomvu alipoisikia akaipenda ikaanza kupigwa,
Diamond akawa anafurahi sana. Safari ya kimuziki ikaanzia hapo na mpaka
sasa mimi ni Official DJ na Tour Manager wa Diamond.






