WAJUE MASTAA WALIOJIKITA KWENYE SIASA

11 years ago133 Views


Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.
Chande abdallah
ILIKUWA
kama kitu cha ajabu baada ya mastaa wa fani mbalimbali nchini hasa wa
muziki na filamu, kutangaza nia zao za kujiingiza kwenye masuala ya
siasa ambapo mpaka sasa mastaa kama Profesa Jay na Afande Sele wameweka
wazi nia zao huku mastaa kama Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye ni Mbunge wa
Mbeya Mjini na Vicky Kamata ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum wakiwa ni
baadhi ya mastaa waliotinga bungeni tangu uchaguzi uliopita.
Bongo siyo nchi pekee ambayo suala hilo limejitokeza, bali hata kwenye
nchi mbalimbali za Afrika, Ulaya na Marekani limewahi kutokea ambapo kwa
nyakati tofauti mastaa wakubwa wamewahi kujitokeza kuwania nafasi
mbalimbali huku wengine wakishindwa na wengine kushinda nafasi za
kuwakilisha wananchi katika nyadhifa mbalimbali. Wafuatao ni baadhi ya
mastaa wakubwa wa majuu ambao wamewahi au wanaendelea kushiriki kwenye
siasa:-
ARNOLD SCHWARZENNEGGER.

ARNOLD SCHWARZENNEGGER
Huyu
ni staa mkubwa wa filamu za ‘action’ nchini Marekani ambaye anajulikana
sana kwa umbo lake kubwa. Jamaa alianza kama mtunisha misuli na kuingia
kwenye tasnia ya filamu ambapo alifanya vema na muvi zake kama
Terminator na Predator. Arnold alianza siasa mwaka 2003 ambapo aligombea
ugavana wa Jimbo la Calfornia na kushinda, alishikilia nafasi hiyo hadi
mwaka 2011.

ANDRIY CHEVSHENKO.

ANDRIY CHEVSHENKO
Ni
msakata kabumbu raia wa Ukraine ambaye alipata mafanikio makubwa katika
historia ya soka duniani ambapo alichezea klabu kubwa duniani kama AC
Milan na Chelsea. Alitangaza kustaafu mwaka 2012 baada ya kucheza soka
kwa muda mrefu. Baada ya kustaafu alijiunga na Chama Cha Demokrasia cha
Ukraine akigombea nafasi ya ubunge, hata hivyo alishindwa kupata nafasi
hiyo kutokana na ushindani mkubwa uliojitokeza.

WYCLEF JEAN

WYCLEF JEAN
Ni
staa wa muziki toka Marekani aliyehamia nchini humo akiwa na familia
yake kama wakimbizi waliotokea nchini Haiti. Jamaa aliwika na ngoma zake
kama 911, Two Wrongs na Hips Don’t Lie aliyoshirikiana na Shakira.
Jamaa alijitosa kwenye siasa mwaka 2010 akitangaza kugombea nafasi ya
urais katika nchi yake ya kuzaliwa ya Haiti ambapo hata hivyo alitolewa
kwenye kinyang’anyiro hicho kutokana na sababu za makazi yaani kuishi
Marekani zaidi kuliko Haiti.

YOUSSOU N’DOUR.

YOUSSOU N’DOUR
Huyu
ni staa mkubwa zaidi Afrika ambaye anatajwa kushika namba moja kwenye
orodha ya wasanii wa muziki matajiri Afrika huku Jarida la Rollingstone
likimtaja kama mwanamuziki anayejulikana sana Afrika.

Mwanamuziki
huyu anayejulikana Afrika na duniani kwa kibao chake cha Dirima,
alitangaza nia ya kugombea urais mwaka 2012 lakini akatolewa kwenye
kinyang’anyiro hicho kutokana na saini za wadhamini wake kuwa na kasoro
na pia kutokana na ushawishi wake aliteuliwa kuwa Waziri wa Utalii na
Utamaduni ambapo anaendelea na nafasi hiyo hadi hivi sasa.

MANNY PACQUIAO.

MANNY PACQUIAO
Jina
lake kamili ni Emmanuel Dapridran Pacquiao ni mkali wa ndondi tokea
Ufilipino mwenye heshima na mafanikio makubwa duniani kwa ujumla. Pamoja
na mafanikio yake alitangaza kujiingiza kwenye siasa mwaka 2007 lakini
alishindwa kiti cha baraza la uwakilishi katika Jimbo la Manila na mwaka
2009 aliamua kugombea tena kupitia Jimbo la Sarangani ambapo alishinda
kwa kishindo kikubwa bila pingamizi chochote ambapo pamoja na masuala ya
ngumi anaendelea kushika nafasi hiyo hadi hivi sasa

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.