
ARNOLD SCHWARZENNEGGER.
ARNOLD SCHWARZENNEGGER
Huyu
ni staa mkubwa wa filamu za ‘action’ nchini Marekani ambaye anajulikana
sana kwa umbo lake kubwa. Jamaa alianza kama mtunisha misuli na kuingia
kwenye tasnia ya filamu ambapo alifanya vema na muvi zake kama
Terminator na Predator. Arnold alianza siasa mwaka 2003 ambapo aligombea
ugavana wa Jimbo la Calfornia na kushinda, alishikilia nafasi hiyo hadi
mwaka 2011.
ANDRIY CHEVSHENKO
Ni
msakata kabumbu raia wa Ukraine ambaye alipata mafanikio makubwa katika
historia ya soka duniani ambapo alichezea klabu kubwa duniani kama AC
Milan na Chelsea. Alitangaza kustaafu mwaka 2012 baada ya kucheza soka
kwa muda mrefu. Baada ya kustaafu alijiunga na Chama Cha Demokrasia cha
Ukraine akigombea nafasi ya ubunge, hata hivyo alishindwa kupata nafasi
hiyo kutokana na ushindani mkubwa uliojitokeza.
WYCLEF JEAN
Ni
staa wa muziki toka Marekani aliyehamia nchini humo akiwa na familia
yake kama wakimbizi waliotokea nchini Haiti. Jamaa aliwika na ngoma zake
kama 911, Two Wrongs na Hips Don’t Lie aliyoshirikiana na Shakira.
Jamaa alijitosa kwenye siasa mwaka 2010 akitangaza kugombea nafasi ya
urais katika nchi yake ya kuzaliwa ya Haiti ambapo hata hivyo alitolewa
kwenye kinyang’anyiro hicho kutokana na sababu za makazi yaani kuishi
Marekani zaidi kuliko Haiti.
YOUSSOU N’DOUR
Huyu
ni staa mkubwa zaidi Afrika ambaye anatajwa kushika namba moja kwenye
orodha ya wasanii wa muziki matajiri Afrika huku Jarida la Rollingstone
likimtaja kama mwanamuziki anayejulikana sana Afrika.
Mwanamuziki
huyu anayejulikana Afrika na duniani kwa kibao chake cha Dirima,
alitangaza nia ya kugombea urais mwaka 2012 lakini akatolewa kwenye
kinyang’anyiro hicho kutokana na saini za wadhamini wake kuwa na kasoro
na pia kutokana na ushawishi wake aliteuliwa kuwa Waziri wa Utalii na
Utamaduni ambapo anaendelea na nafasi hiyo hadi hivi sasa.
MANNY PACQUIAO
Jina
lake kamili ni Emmanuel Dapridran Pacquiao ni mkali wa ndondi tokea
Ufilipino mwenye heshima na mafanikio makubwa duniani kwa ujumla. Pamoja
na mafanikio yake alitangaza kujiingiza kwenye siasa mwaka 2007 lakini
alishindwa kiti cha baraza la uwakilishi katika Jimbo la Manila na mwaka
2009 aliamua kugombea tena kupitia Jimbo la Sarangani ambapo alishinda
kwa kishindo kikubwa bila pingamizi chochote ambapo pamoja na masuala ya
ngumi anaendelea kushika nafasi hiyo hadi hivi sasa






