NCHI za Umoja wa Ulaya zimeahidi kuendelea kusimama pamoja wakati wote ili kuwa taasisi yenye nguvu kubwa duniani baada ya kushuhudia miaka mingi ya migawanyiko ya ndani ikitokea.
Haya yameelezwa kwenye mkutano ambao haukuwa rasmi,uliowakutanisha viongozi 27 ambao ni wanachama wa umoja huo waliokutana katika Mji wa Sibiu ,Romania.
Akizungumza katika mkutano huo, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema ulimwengu haulali na kwa hiyo lazima wawe wabunifu, wawe imara na wawe na umoja.
Na kwamba mpango wa Uingereza kujiondoa katika Umoja huo umeigubika jumuiya hiyo kwa zaidi ya miaka miwili, kwa hivyo mkutano wa jana ulikuwa fursa nzuri ya kutoa mwito wa umoja na kusisitiza kuhusu kanuni za misingi za Umoja wa Ulaya.
Uingereza bado kimsingi ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya lakini Waziri Mkuu Theresa May hakuhudhuria mkutano huo wa kilele wa Romania na akabaki London kujaribu kuupigia debe mpango wake wa Brexit upitishwe bungeni.
CHANZO DW .
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2VaJ62k
via