KIWANDA CHA A TO Z ARUSHA CHAINGIA MKATABA WA MABILIONI KUZALISHA DAWA ITAKAYOTIBU SUMUKUVU KWENYE MAHINDI NA KARANGA

Special Correspondent6 years ago6 Views

Na Seif Mangwangi, Arusha
KIWANDA cha A to Z cha jijini hapa kimeingia mkataba wa bilioni 3.5 wa kuzalisha dawa aina ya AFLASAFE ya kutibia mazao yanayosababisha sumukuvu inayopatikana kwenye mahindi na karanga na ambayo imekuwa ikisababisha maradhi ya saratani ya ini.
Mbali ya saratani ya ini, Sumukuvu (AFLATOX), inaelezwa kusababisha kudumaa kwa watoto ambao wamekuwa wakinywa uji unaotumia unga unaotengenezwa kwa zao la mahindi pamoja na karanga kwaajili ya lishe
Mtendaji Mkuu wa A to Z, Kalpesh Shah na Kaimu Mkurugenzi wa taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mazao ya kilimo (IITA) yenye makao yake makuu nchini Nigeria, Dkt Kenton Dashell walisema dawa hiyo itakuwa ni suluhu ya maradhi ya saratani kwa kuwa yamekuwa yakisababisha vifo vingi kwa wananchi wa Afrika.
DKT Dashell alisema kila mwaka maelfu ya waafrika wamekuwa wakipoteza maisha kwa maradhi yanayosababishwa na sumukuvu na kupoteza nguvu kazi ya mataifa mengi ya Afrika, hivyo kuzalishwa kwa dawa hiyo kutapunguza vifo na kukuza uchumi wa Afrika.
“ Kati ya kampuni nyingi zilizotenda kuomba mradi wa kuzalisha dawa hii, ni A to Z pekee ndio iliyoonekana kuwa na sifa na uwezo wa kuizalisha, kwa hiyo nipende tu kuwapongeza  sana kwa kushinda tendaII H,”alisema.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa A to Z, Kalpesh Shah alisema kampuni yake itatumia Bilioni 3.5 katika mradi huo na kwamba dawa  hiyo itakayokuwa ikijulikana kama Aflasafe TZ01, itaanza kutumika nchini Novemba mwaka huu baada ya uzalishaji kuanza rasmi.
Alisema kwa miaka mingi A to Z imekuwa ikifanya utafiti wa kugundua dawa ya kutibu Sumukuvu kupitia taasisi yake ya utafiti ya ATRC, kwa kuwa sumu hiyo imekuwa ikiwasababishia wakulima hasara kubwa pamoja na kupoteza soko la mazao yao nje ya nchi, hivyo kugunduliwa kwa dawa hiyo na wao kupata fursa ya kuizalisha ni jitihada za muda mrefu za kuokoa vifo na kukuza uchumi wa Tanzania na Afrika.

  Mtendaji Mkuu wa A TO Z Kalpesh Shah akitambulisha dawa aina ya Aflasafe ambayo itatumika kunyunyiziwa kwenye mahindi na karanga kwaajili ya kuua sumukuvu ambayo imekuwa ikisababisha maradhi ya saratani ya ini.
Kaimu Mkurugenzi wa taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mazao ya kilimo (IITA), Dkt Kenton Dashell pamoja na Mtendaji Mkuu wa ATOZ Kalpesh Shah wakibadilishana nyaraka za makubaliano ya kuanza uzalishaji wa sawa aina ya Aflasafe kwaajili ya kuua sumukuvu.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2WDWRbi
via

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...