Tukio hilo lilitokea hivi karibuni nyumbani kwa Nasibu Abdul ‘Diamond’, aliyekuwa akisherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa ndipo wambeya walipoanza kumsengenya Shilole chinichini.“Huyu atakuwa kanasa si bure,” alisikika mmbeya mmoja ambaye hakujitambulisha.
Alipoulizwa Shilole kama ni kweli amenasa ‘kibendi’, alijibu:
“Jamani sina mimba, watu watambue tu kwamba hiyo picha nilikuwa nimetoka kula, lakini pia wajue kwamba siku nikipata mimba watajua tu maana nitapiga picha za kutosha,” alisema Shilole.




































