Stori: Brighton Masalu na Musa Mateja
KUPITIA baadhi ya vijana walio chini ya kundi lake la Wasafi Classic Baby (WCB), âkichaaâ wa Bongo fleva, Nasibu Abdul âDiamond Platnumzâ amepelekea zawadi ya keki, staa wa filamu za Kibongo, Rose Donatus Ndauka alipokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Msanii chipukizi wa lebo ya Wasafi Classic Baby âWBCâ aitwaye Harmonizer akilishwa keki na Rose.Ishu hiyo ilijiri Jumatano iliyopita ndani ya Ukumbi wa Jozi Village, Msasani jijini Dar ambapo vijana hao wa Diamond wakiongozwa na msanii ambaye anasimamiwa muziki na Diamond, Hamonizer, walitinga ukumbini hapo wakiwa wameshikilia boksi lililokuwa na keki, maalum kwa ajili ya Rose.
Oscar Ndauka akilishwa keki na Rose Ndauka ambaye ni mtoto wa kaka yake
Muda wa kula keki ulipowadia, mbali na rafiki wengine kumuandalia muigizaji huyo keki, Kundi la Wasafi Classic Baby lilifunua keki yao ikiwa na maandishi ya âHappy Birthday Rose Ndauka, from Wasafi Classic Baby (WCB)â ambapo walianza kumlisha huku minongâono na miguno ikianza kusikika miongoni mwa wageni waalikwa.
Baadhi ya maneno na fununu ambazo zilitawala ukumbini humo ni kuwa zawadi hiyo ya keki iliandaliwa na Diamond ambaye kwa sasa ni mtu wake wa karibu lakini hapendi watu wajue ndiyo maana akawatuma Wasafi wamuwakilishe sambamba na dada yake, Darleen Abdul âQueen Darleenâ.
Baada ya tukio hilo, waandishi wetu âwalimbananisha ukutaniâ Rose kwa lengo la kutaka kujua lipi ni âtui na yapi ni maziwaâ juu ya madai hayo, alingâaka na kusema yeye na Diamond ni marafiki hivyo si ajabu kuona vijana wake wakimletea zawadi.
âJamani, mbona tunafuatiliana sana? Kwani mimi kupewa keki na vijana wa Diamond ni tatizo? Hii ni sherehe, mtu yeyote hata nyinyi mnaweza kunipa zawadi, niacheni nifurahie kuzaliwa kwangu,â alisema Rose.
Sherehe hiyo iliyofana vilivyo kwa watu kunywa na kula, mastaa mbalimbali walihudhuria akiwemo Jacqueline Wolper, Hamisa Mobeto na prodyuza, Emmanuel Sewando âManeckyâ
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






