TIMU 4 ZA UINGEREZA ZAWEKA REKODI YA KABUMBU BARANI ULAYA

Special Correspondent6 years ago93 Views


 Usuli:
UINGEREZA imefanikiwa kuingiza miamba 4 ya kabumbu ( LIVERPOOL FC, TOTTENHAM HOTSPURS, ASENALI na CHELSEA), kwenye fainali ya vikombe vikubwa viwili vya kabumbu yaani Uefa Champions League na Uefa Europa League.
LIVERPOOL FC ilianza kuonesha njia jumanne pale machinjioni Anfield ilipoipa kipigo cha mbwa mwizi BARCELONA kwa kuitandika mabao 4-0, huku LIONEL MESSI akiwekwa mfukoni na beki bora duniani, VIRGIL VAN DIJK.
TOTTENHAM ilifuata nyayo jumatano kwa kuikung’uta AJAX mabao 3-2 pale Amsterdam arena, huku Mbrazil LUCAS MAURA akitupia kambani Hat-trick ya kufa mtu.

Usiku wa Alhamis, ASENALI ikiwa pale uwanja wa Mestalla iliibuguza Valencia 4-2 huku Mwafrika mwenye uwezo usio wa kawaida wa kupachika mabao, PIERRE EUMERIC AUBUMEYANG “Auba”, akitakata vilivyo.

Usiku huo huo, CHELSEA iliibuguza Entratch Frankfurt mabao 4-3 kwa mikwaju ya penati huku nyanda KEPA ARRIZABALAGA akiibuka shujaa kwa kunyaka mikwaju ya penati.

2. Rekodi Mpya Ulaya:
UINGEREZA, kwa kuingiza timu hizo nne kwenye michuano hiyo miwili, imeweka rekodi mpya barani Ulaya kwa nchi moja kuingiza timu zote 4 kwenye makombe 2 makubwa barani humo. Hii ni kwavile hakuna nchi yoyote iliyowahi kufanya hivyo.

3. Mitanange 3 ya Kufa Mtu:
3.1 ASENALI Vs CHELSEA:

Tarehe 28 Mei 2019 kwenye uwanja wa Olyimpic stadium, jijini Baku, Azerbaijan, utapigwa mtanange wa kuwania mshindi wa Uefa Europa League kati ya Majogoo hao wawili wa London.

3.2 LIVERPOOL FC VS TOTTENHAM:

Tarehe 1 Juni 2019, dunia itasimama ambapo mabilioni ya manazi wa kabumbu duniani watashuhudia mtanange huu wa kukata na shoka utakaopigwa Estado Metropolitan, Hispania huku BBC tayari ikiipa LIVERPOOL FC 70% ya kunyakua ndoo hiyo na TOTTENHAM 30%.

3.3 UEFA Super Cup:

Mtanange mwingine utakuwa tarehe 1 Agosti 2019 ambapo mshindi wa Uefa Champions League atakipiga na mshindi wa Uefa Europa League jijini Instabul, Uturuki.
4. ASENALI Kucheza Champions League?

Uingereza ina nafasi 4 za Champions league msimu ujao ambazo tayari zimechukuliwa na MAN CITY, LIVERPOOL FC, CHELSEA na TOTTENHAM.

Timu inayoshinda kombe la Uefa Europa League hupata nafasi ya kucheza Champions League. Kwa maana hiyo, iwapo ASENALI itaitandika CHELSEA pale Baku, basi itapata nafasi ya kucheza Champions League msimu ujao. Hii inamaanisha Uingereza itakuwa na timu 5 kwenye Champions league msimu ujao. Hata hivyo, iwapo CHELSEA itaifunga ASENALI, basi Uingereza itabaki na timu 4.

5. MANCHESTER UNITED YATOWEKA DUNIA YA KABUMBU!!!

MANCHESTER UNITED ni timu yenye wapenzi wengi kuliko timu zote duniani na timu yenye manazi wenye mikwara na ngebe kuliko manazi wa timu zote duniani!. Hili lilidhihirika miaka ya nyuma na kujirudia Januari 2019, ilipokuwaikishinda mechi mfululizo huku MARKUS RASHFORD na “Mmasai” OLE GUNNAR SOLSKIER wakitangazwa Mchezaji na Kocha Bora wa Mwezi na PAUL POGBA akisifiwa kuwa ni “mchezaji wa kipekee duniani” ambapo magazeti na mitandao ya kijamii ilitamalaki mbwembwe na nyodo za kila aina za manazi wa MAN U huku wenye “Vibanda umiza” wakiingiza faida kubwa kutokana na wapenzi hao wenye ngebe kufurika hadi pomoni vibandani humo!.
MANCHESTER UNITED sasa imekuwa ni “endangered species” yaani viumbe vinavyotarajiwa kutoweka duniani!. Itamchukua “Mmasai” OGS miaka 10 kuifufua MAN U. Manazi wa MAN U sasa wamebakia kushabikia timu za wapinzani kama ilivyokuwa katika mechi ya LIVERPOOL VS BARCA ambapo waligeuka kuwa Mashabiki wa Mkopo wa Barca na kuishia kurudi makwao vichwa chini!. Hayo ndio yatakuwa maisha yao kwa muongo mmoja ujao!!!.

KONGOLE Liverpool Fc, Tottenham, Asenali na Chelsea👏👏👏
“In England, the level is very high and the Premier League is the best competition in the world that is why the four English clubs have created European football history by taking all four final spots in the continent’s two major competitions”.

MAURIZIO SARRI, 9 Mei 2019.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2Jalv0h
via

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.