SHEIKH MTUPA AWATAKA WANAOJIWEZA KIMAISHA KUSAIDIA WASIOJIWEZA NA WENYE MATATIZO

Special Correspondent6 years ago4 Views

NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA

SHEIKH wa Mkoa wa Pwani,Khamis Mtupa ametoa rai kwa jamii inayojiweza kimapato,  kujitolea kuwasaidia watu wenye matatizo na wasiojiweza kwani ni njia mojawapo ya kujitengenezea na kujihifadhia twawabu ya kuingia peponi.

Aliyasema hayo wakati akifungua umoja wa Twariqa ,wilayani Kibaha ambazo ofisi yake ipo kata ya Kongowe Mtaa wa Mwambisi.

 Sheikh Mtupa aliwaeleza waumini wa dini ya kiislamu na wananchi kuwa mwanadamu akijihusisha na wenzake katika Twariqa ya kujitolea kusaidia wasiojiweza hujiandalia pepo. 

“Umoja huu wa twariqa ulioanzishwa mtaa wa Mwambisi kila anayeingia basi afahamu Twariqa inachukua dhamana ya yeye kufika peponi In jehanam firdaus Pepo ambayo kama tunazungumzia matokeo ya mtihani basi huyo mwanafunzi anakuwa amepata daraja la kwanza, 

“Hivyo ndugu zangu waislamu na wananchi kwa ujumla tujumuike na wenzetu katika umoja huu wa Twariqa ambao upo mahususi kwa ajili ya kusaidiana” alisema sheikh Mtupa.

Nae sheikh wa wilaya ya Kibaha,Said Mtonda alieleza, lengo la kuanzishwa kwa umoja huo wa Twariqa kwa wilaya ya Kibaha ni umoja wa kushirikiana kwa waumini wa dini ya kiislamu na wananchi katika kutoa msaada kwa waislamu wenzao na jamii pindi wanapopatwa na matatizo jambo la furaha.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2vMMGFL
via

Previous Post

Next Post

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...