Mkuu Wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakishirikiana na mkuu wilaya ya Arumeru jana wamegawa vitambulisho vya kufanya biashara kwa wafanya biashara wadogo wadogo (machinga) hii ikiwa ni awamu ya pili yaugawaji.
Mkuu wa mkoa huyo pia alikabidhi wilaya ya Arumeru vitambulisho vya machinga Elfu kumi ambavyo vitagawiwa kwa halmashauri mbili zilizopo ndani ya wilaya ya Arumeru ambapo kila halmashauri imekabidhiwa vitambulisho 5000.
Akizungumza kuhusiana na ugawaji huo, Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro alisema kuwa hii ni awamu ya pili ya ugawaji wa vitambulisho ,
Alisema kwa jana tu katika soko la Tengeru wamegawa vitambulisho 1000 kwa wafanyabiashara na wataendelea kuvigawa Hadi wafanyabiashara wote wavipate
“kama mnavyoona mimi na timu yangu yote tumeingia sokoni na tumefanyakazi mmeona watendaji wangu wa kata wafanyakazi wa halmashauri wote bila kujali cheo tumeingia kugawa vitambulisho vya machinga na tumegawa vitambulisho 1000 natunaendelea kugawa katika masoko yote”alisema Muro
Alimshukiru mkuu wa mkoa wa Arusha kwenda kuwapa ushirikiano katika zoezi hilo kwani amewapa motisha ya kutosha.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Ariana Mrisho Gambo alisema ameamua kuwapamotisha ya ugawaji wa vitambulisho wafanyakazi wa wawilaya hiyo.
Picha ikionesha Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro wa kwanza kulia akimkabidhi mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha Dr. Wilson Mahera vitambulisho 2500 Kwa ajili ya kuwagawia wafanyabiashara wadogo wa halmashauri yake
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2GY4a6Z
via