HEBU ANGALIA WEMA SEPETU NA PENNY WAKIMKEJELI DIAMOND NA ZARI THE LADY BOSS

Admin Updates11 years ago77 Views


Stori: Imelda Mtema
Mastaa wawili hapa Bongo ambao huko
nyuma walikuwa katika bifu kali, Wema Sepetu na Penny Mwingilwa
wameonekana kumkejeli aliyekuwa mpenzi wao, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa
kutumia neno Project.



Mastaa hao walionekana wameweka picha
yao wakiwa pamoja wamejilaza chini nyumbani kwa Wema  na kuandika kuwa
wakiwa katika Project yao neno ambalo lilitumiwa na Diamond akiwa na
mwanadada Zarina Hassan  ‘Boss lady’ anayedaiwa kutoka kimapenzi na
mwanamuziki huyo.



Gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na
Penny kwa njia ya simu ambapo alisema kuwa siku hiyo walikutana na
kuzungumza na rafiki yake huyo wa muda mrefu na mambo ya project
yalitokea tu.

“Sisi tulimisiana sana na tulikutana na kuzungumza mambo mengi ya zamani, hiyo project iliingia tu,” alisema Penny.
GPL

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...