DAN ALVES:MESSI NI BORA, HATA ASIPOPATA TUZO

12 years ago125 Views

article-2274726-17648C8F000005DC-173 634x5371 21a9d

MLINZI wa kulia wa Barcelona, Dan
Alves amedai kuwa anaamini Lionel Messi ataendelea kuwa mchezaji bora
zaidi kwa sasa ulimwenguni hata kama hatapata tuzo ya mwanasoka bora wa
dunia. 


Mastaa Cristiano Ronaldo wa Real
Madrid na Franck Ribery wa Bayern Munich wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa
tuzo hiyo, lakini Alves anaamini kuwa haitabadilisha lolote na Messi
ataendelea kuwa mchezaji bora zaidi wa zama hizi.

“Tuzo ya mwanasoka bora wa dunia
inachosha kidogo kwa sababu imehamishwa mahala pake. Imepelekwa katika
eneo la mawazo ya watu, nje ya uwanja wa soka. Lakini kama tukitazama
mambo ya uwanjani nadhani Lionel anawasukuma wengine katika nafasi ya
pili,” alisema Alves.

Kwa misimu minne mfululizo, Messi
amechaguliwa kuwa mwanasoka bora wa dunia na ingawa msimu huu hapewi
nafasi kubwa kutokana na kuwa majeruhi kwa kipindi kirefu, lakini bado
amechaguliwa katika orodha ya wachezaji watatu wanaowania tuzo hiyo.
Chanzo: mwanaspoti

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.