PENNY: MITANDAO ILITAKA KUNITOA UHAI WANGU..KWA SABABU HII…..

Admin Updates10 years ago7 Views

Ndani ya safu hii leo tunakutana na
Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’ ambaye yuko kimya katika masuala ya
utangazaji tangu alipoamua kuondoka Radio E FM.
Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’.Msikilize Penny alipobanwa kwa maswali kumi na Mwandishi Wetu Imelda Mtema.
Ijumaa: Upo kimya sana shosti, ni nini unachofanya kwa sasa?
Penny:
Sasa hivi mimi ni mbunifu wa mpangilio wa nyumba na ofisi ambapo
namshauri mtu aiwekeje nyumba yake katika muonekano mzuri wenye mvuto
pamoja na ofisi kwa ujumla.

Ijumaa: Mambo ya utangazaji umeachana nayo au una mpango wa kusaka kazi sehemu nyingine?
Penny:
Unajua hakuna kitu kizuri kama mtu kuwa na taaluma yako kichwani, yaani
hata kama nitakaa miaka kumi bado fani yangu itakuwa ni utangazaji.

Ijumaa: Kuna tetesi kuwa ukikasirishwa tu na mpenzi unakimbilia kunywa sumu, ni kweli?
Penny: (kicheko) Hao wanaosema hivyo watakuwa wananijua sana kuliko mama yangu, siko hivyo wanavyodai jamani.
Ijumaa: Mwanaume ambaye uliamua kumuweka wazi alikuwa ni Diamond tu, kwa nini sasa hivi unaficha?
Penny: Unajua kuna mwanaume mwingine hapendi mambo ya kujulikana kwani wote siyo mastaa.

Ijumaa: Kwa sasa wewe na Wema ni marafiki, je mkikaa huwa hamuongelei mambo ya mpenzi wenu aliyepita?
Penny: Hakuna kitu kama hicho, sisi huongelea mambo yetu binafsi kwani urafiki wetu ni tangu kitambo.
Ijumaa: Kuna kipindi ulivalishwa pete ya uchumba na ulikuwa mbioni kuolewa, ilikuwaje?

Penny: Ni kweli na lengo bado liko palepale, ikifika muda nitaolewa kwani sijatangaza kama tumeachana.
Ijumaa: Kuna kipindi ulikutana na mtihani kupitia mitandao ya kijamii, ulijifunza nini?
Penny:
Nilichojifunza ni kwamba watu wengi wanaotumia mitandao ya kijamii
wanakurupuka na hawana utu kwani wanaweza kupoteza uhai wa mtu kama
hayuko imara.

Ijumaa: Ulishafikiria kutoa uhai wako kwa ajili ya mitandao ya jamii?
Penny:
Nilishawahi kuwaza nijiue lakini namshukuru sana mama yangu aliniambia
kuwa hakuna kitu ambacho hakiwezi kuisha hata siku moja.

Ijumaa: Unazungumziaje bifu la Kajala na Wema?
Penny:
Mimi ninachojua wale ni marafiki wanaopendana sana, ipo siku tofauti
zao wataweka pembeni kwa sababu siku hizi hakuna haja ya kuwekeana
mabifu.

Ijumaa: Ulishawahi kwenda kwa mganga kwa kusaka mafanikio au jambo lolote?
Penny:
Siku zote katika maisha yangu mganga wangu ni Mungu maana ananijibu kwa
haraka sana, sijawahi kumtegemea mganga wala hilo halitatokea.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.