WAZIRI WA MAMBO YA NJE AZUNGUMZA NA MKURUGENZI WA AFRIKA KUTOKA NORWAY

Special Correspondent6 years ago6 Views

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Kusini mwa Afrika kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Norway, Bw. Germund Saether. Katika mazungumzo hayo, walijadili umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Norway hususan katika sekta za kukuza uchumi kwa maendeleo ya mataifa haya mawili. Mazungumzo hayo yamefanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam tarehe 10 Mei 2019 
Kulia ni Balozi wa Norway hapa nchini, Mhe. Elisabeth Jacobsen pamoja na maafisa kutoka ubalozi huo wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi na mgeni wake (hawapo pichani). 
Mazunguzmzo kati ya Mhe. Prof. Kabudi na Bw. Saether yakiendelea huku wajumbe wengine wakifuatilia. Pembeni kwa Mhe. Prof. Kabudi ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestas Nyamanga pamoja na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo 
Picha ya pamoja 
Prof. Palamagamba John Kabudi akiagana na Mgeni wake. 

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2vOCkVE
via

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...