WAZIRI PROFESA NDALICHAKO:UDSM IMEONA MBALI KATIKA KUWEKEZA KWENYE UTAFITI WA MATATIZO YA WANANCHI.

Special Correspondent6 years ago6 Views

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameupongeza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) kwa kutenga sh. bilioni moja kwa ajili ya kuwawezesha wanataaluma kufanya tafiti zaidi hasa zinazogusa matatizo ya jamii moja kwa moja.

Waziri Ndalichako ametoa pongezi hizo jijini Dar es Salaam wakati akifunga maadhimisho ya tano ya Wiki ya Utafiti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo amesema tafiti ni muhimu katika kuleta maendeleo kwa kujenga na kukuza uchumi wa viwanda nchini.

Prof. Nalochako amesema serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda lengo likiwa kuhakikisha kunakuwa na viwanda ambavyo vinatumika kuzalisha bidhaa na kutoa huduma zitakazotosheleza jamii ya Kitanzania na kusaidia kuongeza ajira kwa vijana.

Akizungumzia Wiki ya Utafiti Waziri Ndalichako amesema inawapa wadau wa utafiti na ubunifu jukwaa la kufahamu shughuli za utafiti zinazofanyika; sehemu gani kuna mapengo na changamoto; na mikakati gani ya kimipango inahitajika ili kuziba mapengo pamoja na kutatua changamoto zilizobainika.

“kama taifa, tuna wajibu mkubwa na fursa nyingi za kuweza kutumia utafiti, ubunifu na ujasiriamali hususan kupitia sekta ya elimu ili kuongeza kasi ya maendeleo ya viwanda nchini. Kufanya hivyo, kutawezesha kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Dira ya Taifa ya 2015, ya kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia uchumi wa kati kupitia viwanda.” Amesisitiza Waziri Ndalichako.


Nae Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa William Anangisye amesema kuwa tafiti zinazofanyika zinafanya Chuo kuweza kutambulika kimataifa.

Amesema wanataraji kutenga sh.bilioni moja kwa ajili ya kazi za utafiti ili kuweza matokeo katika maendeleo katika utengenezaji sera mbalimbali.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho amesema kuwa tafiti ndizo kiungo na serikali katika kusaidia wananchi kutatua changamoto mbalimbali.

 Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akipata maelezo katika maonesho ya Utafiti katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akifunga wiki ya Tano ya Utafiti wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) uliofanyika katika ukumbi wa Nkrumah wa Chuo hicho.

 Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam -Profesa William Anangisye akitoa maelezo kuhusiana na Wiki ya Tano ya Utafiti wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
 

 Baadhi ya wadau katika wiki ya Tano ya Utafiti wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2vOpR4d
via

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...