WANYAMBLIS TOTTENHAM WANA ASILIMIA KUBWA YA KUTWAA NDOO YA CHAMPIONS LEAGUE!!!

Special Correspondent6 years ago5 Views


TOTTENHAM HOTSPURS imeonesha kabumbu la kuvutia sana katika Champions league ya mwaka huu na kwa hakika kuna kila dalili ya kutwaa ndoo ya Champions Lg pale Estadio Metropolitan, Madrid Juni 1, 2019.

Katika michuano hii, SPURS ilipangwa kundi gumu lililowajumuisha Barca na ilipigwa mechi 3 za mwanzo lakini ikakomaa hadi kupenya!

SPURS iliwatandika Mabingwa wa Uingereza MAN CITY ambao wao ndoo ya Champions league miaka nenda miaka rudi wanaitazamia runingani tu!. Halikuwa jambo rahisi.

SPURS imewatoa AJAX timu iliyowavua ubingwa Real Madrid na Juventus iliyo na Mnyama CHRISTIANO RONALDO.

SPURS ikiwa na kocha wa kiwango cha juu, MAURICIO POCHETINO, imekuwa ikipiga kabumbu la uhakika na hainaga ujinga wa kupaki basi unaoboa maelfu ya watazamaji uwanjani na mamilioni runingani!

SPURS wana nafasi kubwa sana ya kunyakua ndoo hiyo ya CL hasa kwavile inakutana na JURGEN KLOPP’s LIVERPOOL.

KLOPP ana gundu kubwa na fainali kwani katika fainali zake 7 akiwa Borrusia Dortmund na Liverpool, ameshinda moja tu na kuangukia pua katika fainali SITA!!.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2HcoZwS
via

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...