SHIRIKISHO LA WALIMU MAKADA WA CHAMA CHA MAPINDUZI WAKABIDHI MIFUKO 120 YA SARUJI.

Special Correspondent6 years ago5 Views

Na Shushu Joel, Mkuranga. 

MBUNGE wa jimbo la Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega ambaye pia ni Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi amepokea msaada wa mifuko 120 ya saruji kutoka kwa shirikisho la walimu makada wa chama cha mapinduzi  (CCM).

Akizungumza wakati wa kukabidhi mifuko hiyo mratibu wa shirikisho hilo  Bakari Msingili alisema kuwa kusudi la wao kufanya uamuzi huo ni kutokana na juhudi za kimaendeleo  zinazo fanywa na Mbunge huyo  kwenye nyanja za elimu,Afya na miundombinu kwenye wilaya ya mkuranga.

Aliongeza kuwa imekuwa  ngumu kuamini kwa kile ambacho tunakifanya kama walimu juu ya kuchangia fedha kwa ajili ya maendeleo kutokana na tabia iliyojengeka kwa watu kuwa walimu ni kundi la watumishi ambao ni wabaili  sana.

“Mifuko hii ya saruji itasaidia kwenye nyanja hii ya elimu lakini hata sie kama shirikisho la walimu makada wa ccm” Alisema Bakari.

Naye Afisa elimu ya watu wazima  Mektrida  Kahindi ambaye ni mjumbe wa shirikisho hilo alisema kuwa shirikisho hilo litaendelea kutoa  misaada mbalimbali katika wilaya hiyo kwa lengo la kusaidia maendeleo kwenye wilaya ya mkuranga.

Aliongeza kuwa mifuko hii ya 120 ya saruji ni mwanzo tu lakini kuna mambo makubwa ya nakuja mbele yetu.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo Ulega  amewapongeza wana shirikisho hilo kwa kutambua juhudi wanazozifanya  jimbo humo hivyo amewataka wananchi wake kutumia  kwa uangalifu saruji hizo kwani mwezi wa kumi  watakuja  ili kuhakikisha usahihi wa kazi jinsiilovyoondoka


Aidha Ulega amewapongeza walimu hao kwa kuridhishwa na kuona kile kinachofanwa na Serikali ya awamu ya tano china ya Rais Dkt John Pombe Magufuli. 

Aidha Ulega amewataka walimu kuunda vikundi ili kupata mikopo ya wanyama kama ng’ombe na mbuzi ili waweze kuwaingizia kipato cha ziada mbali na kutegemea mshahara.
 Mbunge  wa jimbo la Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi  (wapili kuliua )akipokea  mifuko 120 ya saruji kutoka kwa shirikisho la walimu makada wa chama cha mapinduzi  (CCM)(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mkuu wa wilaya ya  Mkuranga Filberto Sanga kulia na Mbunge  wa jimbo la Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (wapili kulia) wakiwapongeza  walimu makada wa chama cha mapinduzi  (CCM kwa  kukabidhi   mifuko 120 ya saruji.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2WxzWyo
via

Previous Post

Next Post

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...