Mrembo Tunda Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Tetesi Kuwa Wameachana na Yound D

10 years ago108 Views

Mrembo ambaye amewahi kung’arisha vichupa kadhaa vya mastaa Bongo maarufu kama Tunda amekuwa akitajwa kutoka kimapenzi na rapa kijana maarufu kama Young D au Paka Rapper.
Hivi karibuni kuna uvumi ulizuka kuwa wawili hao wameacha baada ya mrembo huyo kufuta baadhi ya picha alizowahi kupiga na Young Dee huku kati ya zaidi ya picha 480 zilizopo kwenye ukurasa wake wa Instagram amebakiza picha moja tu ya rapa huyo.
Vilevile katika ukurasa wa Young Dee kati ya picha 125 alizowahi kupiga na mrembo huyo wa vichupa ameiacha picha moja tu, jambo ambalo limeibua maswali mengi kwa wapenzi wa burudani wanao wafuatilia mastaa hao.
Kupitia kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio mrembo huyo wa vichupa amefungukia suala hilo na kueleza  kuwa yeye na Young Dee wapo sawa ingawa kuna baadhi ya maneno yake yaliashiria kuwepo jambo analolificha.
Alipoulizwa kama yeye na Young Dee ni wapenzi alijibu.”ndiyo Mimi na Young Dee tulikuwa wapenzi”, huku kitendo hicho cha mastaa hao kufuta picha limekuwa ni jambo ambalo linawatokea mastaa wengi pindi kunapotokea tofauti kati yao.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.