MASELE AIKINGIA KIFUA SERIKALI YA TANZANIA KWENYE BUNGE LA AFRIKA

Special Correspondent6 years ago82 Views

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akisisitiza jambo wakati akiongoza kikao cha Bunge la Afrika leo Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.Picha na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuchukua hatua za haraka kusaidia nchi za Kusini mwa Afrika (Msumbiji,Malawi na Zimbabwe) zilizoathirika na Kimbunga cha Idai. 
Mheshimiwa Masele ambaye pia ni Mbunge wa Shinyanga Mjini ametoa pongezi hizo leo Mei 7,2019 akiongoza kikao cha Bunge la Afrika kinachofanyika Jijini Johannesburg,nchini Afrika Kusini wakati wabunge wakijadili kuhusu Ripoti ya kazi ya Umoja wa Afrika (AU). 
Mhe. Masele alilazimika kutoa ufafanuzi baada ya hoja kuibuka hoja bungeni kuwa nchi za Umoja wa Afrika zimekuwa hazichukui hatua za haraka panapotokea majanga mbalimbali. 
ā€œNitumie fursa hii kuipongeza sana serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwa kuchukua hatua za haraka kusaidia chakula na madawa kwa nchi zilizokumbwa na Kimbunga Idaiā€,alisema Mhe. Masele. 
ā€œSerikali ya Tanzania ilikuwa mstari mbele kutoa msaada wa chakula,dawa na vifaa vya kujiihifadhi kwa nchi ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrikaā€,aliongeza Mhe. Masele.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akiongoza kikao cha Bunge la Afrika leo Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akiongoza kikao cha Bunge la Afrika leo Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini. Katikati ni Rais wa Bunge la Afrika, Mhe. Roger Nkodo Dang akitoa taarifa ya kazi ya Bunge la Afrika.
Wabunge wakiwa ukumbini.
Kikao cha bunge kikiendelea.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2PUp5fc
via

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.