MAPENZI:ASILIMIA 75 YA WANAWAKE WAKIRI SMARTPHONES ZIMEPUNGUZA MUDA WANAOTUMIA PAMOJA NA WAPENZI WAO

10 years ago97 Views

Kama simu yako ya mkononi haikatiki kiganjani mwako muda wowote, inaweza ikawa inaharibu uhusiano wako na umpendaye.

Wanasaikolojia wamesema kuwa watu wengi kwa sasa wanalazimika kushindana na smartphone za wapenzi wao kupata attention. Utafiti uliofanywa, umebaini kuwa robo tatu ya wanawake wanaona kuwa smartphones zinaingilia maisha yao ya mapenzi na kupunguza muda ambao wangetumia kuzungumza au kuwa karibu na wapenzi wao
Wanasayansi wamedai kile walichokiita ‘technoference’ kina madhara makubwa kama migogoro mingi, kupunguza quality ya uhusiano, kupunguza mridhisho wa maisha na hatari kubwa ya msongo wa mawazo.
Utafiti huo ulifanywa na mwanafunzi wa chuo kikuu cha jimbo la Pennsylvania, Marekani na mwingine wa chuo kikuu Brigman Young University cha Utah na kuhusisha wanawake 143.
Asilimia 62 walisema teknolojia imeingilia muda waliotumia pamoja na wapenzi wao na theluthi moja wakisema boyfriend zao waliangalia smartphone wakati wakizungumza.
Wanasayansi hao wameshauri kuweka simu silent na kutokuwa nazo muda wote ili kuwa na muda wa kufocus kwa mpenzi wako.
“Kama unataka kuangalia kitu muhimu, toa maelezo kwanza na kisha angalia simu yako. Na pia usijitetee pale mpenzi wako akionesha kukerwa na tabia yako ya kuangalia sms au kucheza games mara kwa mara – ni njia ya yeye kusema kuwa angetaka kuconnect na wewe moja kwa moja,” wamesema.
Chanzo: Daily Mail

Previous Post

Next Post

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.