Man United wachezea kichapo Old Trafford, Haaland atupia bao 2

2 years ago109 Views

 

Wenyeji, Manchester United wamekutana na kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa mahasimu wao wa Jiji, Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.

Mabao ya mabingwa hao wa England na Ulaya yamefungwa na mshambuliaji wake Mnorway, Erling Braut Haaland mawili dakika ya 26 kwa penalti na 49, huku la tatu likiwekwa nyavuni na kiungo Muingereza, Phil Walter Foden dakika ya 80.

Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 24 sawa na Arsenal wakiwa wamefungana hadi kwa wastani wa mabao (GD) katika nafasi ya pili na tatu nyuma ya vinara, Tottenham Hotspur wenye pointi 26 baada ya wote kucheza mechi 20.

Kwa upande wao Mashetani Wekundu baada ya kupoteza mchezo huo wa nyumbani wanabaki na pointi zao 15 za mechi 10 pia nafasi ya nane.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.