MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imebatilisha kifungu cha sheria cha 7(3)kinachowaruhusu Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri kuwa wasimamizi wa Uchaguzi nchini.
Uamuzi huo umetolewa leo Mei, 2019 Uamuzi his na Jaji Atuganile Ngwala kunatokana na kesi namba 8 ya mwaka 2018 iliyofunguliwa na Mwanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Bob Chacha Wangwe.
Aidha katika maamuzi hayo Jaji Ngwala, ametengua kifungu cha 7 (1) kinachoruhusu mtu yeyote kuwa msimamizi wa uchaguzi na kusema kuwa sheria hizo ni batili na kinyume cha katiba ya nchi.
Akisoma uamuzi huo, Jaji Ngwala amesema kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa kwenye mahakama hiyo na mpeleka maombi kuwa wasimamizi wa chaguzi ni wanachama wa chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wanamaslahi kwenye chaguzi hizo.
Mpeleka maombi (Bob) katika kesi hiyo amewakilishwa na Wakili Fatma Karume, ambae aliwasilisha ushahidi wa majina74 ya wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wanachama wa (CCM). Kama ushahidi wa dhidi ya shauri hilo.
Jaji Ngwala amesema kuwa sheria hizo hazijaelekeza utaratibu wowote wa kuhakiki kuwa wasimimizi hawana maslahi binafsi na uchaguzi.
Amesema ya Kuwa sheria hii ya Tume ya Uchaguzi imekataza mtu yoyote ambaye mwanachama wa chama chochote haruhusiwi kuwa msimamizi wa Uchaguzi.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2vTfQmo
via