Maboresha makubwa NSSF

7 years ago109 Views

SHIRIKA la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limesema linaendelea kuboresha mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kwa lengo la kuwahudumia wanachama na wadau wao.

Katika maboresho hayo ambayo yamejikita katika mfumo wa kushughulikia malalamiko, maulizo na maoni ya wanachama wake na wadau wengine wa Shirika.

Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Lulu Mengele, alisema jana, Dar es Salaam, Shirika linawajali wanachama na wadau kwa ujumla katika mawasiliano ambapo mwanachama atapiga namba ya bure 0800756773 kuanzia saa 2.30 asubuhi, hadi 10.30 jioni, Jumatatu mpaka Ijumaa.
“Mwanachama na wadau wetu watapiga namba hiyo bure kabisa kuwasilisha matatizo yao” alisema Lulu.
Alisema kwa kuboresha zaidi utoaji huduma, mwanachama anaweza kuwasilisha malalamiko, maulizo au maoni yake kupitia barua pepe complaints@nsssf.or.tz, 

Alisema Shirika linapenda kuwahakikishia wanachama na wadau kwamba litaendelea kuboresha mifumo yake ya utendaji na utoaji huduma kwa wanachama na wadau wake ili kuboresha na kurahisisha huduma kwa wateja.

from MICHUZI BLOG https://issamichuzi.blogspot.com/2019/03/maboresha-makubwa-nssf.html
via

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.