ETI KUMBE HIKI NDICHO KILICHOMPONZA DIAMOND KWENYE TUZO ZA KILI 2015??… NI HIKI HAPA

10 years ago132 Views


Diamond Platinumz.
Tuzo za Muziki za Kili 2015,
Jumamosi ya wiki iliyopita zilitimua vumbi kwenye Ukumbi wa Mlimani
City, Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo maelfu ya Watanzania wanaopenda
burudani walikuwa wakifuatilia mwenendo mzima wa tuzo hizo, ambapo
msanii Ali Kiba aling’ara baada ya kunyakua tuzo tano na kumuacha mbali
hasimu wake mkubwa, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ aliyeambulia tuzo
mbili tu.
Baadhi ya mastaa walio hudhuria utoaji wa tuzo hizo.
Mpango
mzima ulianza, mishale ya saa tatu za usiku ambapo wasanii pamoja na
wadau mbalimbali walijumuika kwenye zulia jekundu na kupiga
‘mapichapicha’ ya ukumbusho kabla ya mchakato wa kutoa tuzo haujaanza.
Vanesa Mdee na Jux wakifuatilia tuzo hizo kwa karibu.
Baada
ya hapo, pazia la burudani lilifunguliwa na msanii chipukizi, Ruby
anayetamba na ngoma yake ya Na Yule, akafuatiwa na Ommy Dimpoz, baadaye
akapanda jukwaani Barnaba Elias sambamba na Vanessa Mdee, akapanda
Christian Bella kisha Weusi wakiongozwa na Joh Makini na Nikki II
wakafunga pazia la burudani kwa kukamua ile mbaya.
ALI KIBA ANG’ARA
Ali Kiba.
Baadaye
ulifuatia mchakato wa kutoa tuzo ambapo msanii Ali Kiba, alizoa tuzo
tano; Mtumbuizaji Bora wa Mwaka, Wimbo Bora wa Mwaka (Mwana), Mtunzi
Bora wa Mwaka (Bongo Fleva), Wimbo Bora wa Afro (Mwana) na Mwimbaji Bora
wa Kiume (Bongo Fleva) huku hasimu wake Diamond Platinumz akiambulia
tuzo mbili tu; Wimbo Bora wa Zouk/ Rhumba (Nitampata Wapi) na Video Bora
ya Muziki ya Mwaka (MdogoMdogo).
KILICHOMPONZA DIAMOND NI HIKI
Kutokana
na matokeo hayo, inaelezwa kuwa kilichomponza msanii Diamond Platinumz
ni ujumbe wake aliowahi kuutuma kwenye mitandao ya kijamii, akiziponda
Tuzo za Kili kwamba hazizingatii vigezo, kwa kuwaacha wasanii wanaofanya
vyema kwenye tasnia ya muziki na badala yake, ‘kuwapendelea’ baadhi ya
wasanii kutokana na sababu binafsi za waandaaji.
“Unajua Diamond
alikosea sana kuziponda Tuzo za Kili kwa sababu ndizo zilizompaisha
mwaka jana, matokeo yake amempa nafasi mpinzani wake, Ali Kiba kung’ara
kwa kunyakua tuzo kibao, nafikiri atakuwa amejifunza jambo,” alisema
Bruno Sanga, mmoja kati ya wadau waliohudhuria utoaji wa tuzo hizo.
WASHINDI WENGINE
Ukiachilia
mbali Ali Kiba na Diamond, wengine walioziteka tuzo hizo ni mwanadada
Vanesssa Mdee aliyenyakua tuzo mbili; Mtumbuizaji Bora wa Mwaka (Kike)
na Mwimbaji Bora wa Kike (Bongo Fleva), Mzee Yusuph; Mwimbaji Bora wa
Kiume Taarab, Mtunzi Bora wa Mwaka (Taarab) na Kundi Bora la Taarab
(Jahazi).
Wengine ni Jose Mara aliyenyakua tuzo mbili, Isha Mashauzi,
Joh Makini, Baraka Da Prince (Msanii Bora Chipukizi), Nahreel
(Mtayarishaji Bora wa Mwaka) na Mrisho Mpoto aliyeondoka na Tuzo ya
Wimbo Bora Wenye Vionjo vya Asili (Waite).
Sauti Sol walinyakua Tuzo
ya Wimbo Bora wa Afrika Mashariki (Sura Yako), Profesa Jay (Wimbo Bora
wa Hip Hop – Kipi Sijasikia), Jux (Wimbo Bora wa R&B- Sisikii) na
Wimbo Bora wa Bendi wa Kiswahili iliyokwenda kwa FM Academia (Vijana wa
Ngwasuma) na Bendi Bora ya Mwaka (FM Academia) huku Yamoto Band
wakinyakua tuzo ya Kikundi Bora cha Mwaka (Bongo Fleva).

GPL

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.