
Daniel Chongolo na Sanga wateuliwa na CCM Makambako
Kamati kuu ya ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Taifa imewateua Wagombea Wiwili (2)Ndugu Deo Sanga na Ndugu Daniel Chongolo kugombea Ubunge jimbo la Makambako Mkoani Njombe.
Akisoma majina ya Wagombea wa majimbo ya Uchaguzi nchi nzima Katibu wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg.Amos Makalla ametaja Majina hayo leo July 29,2025.
Masama Blog Tunawatakia Kila Heri wateule wote hawa Ndugu Sanga na Ndugu Chongolo katika kuomba ridhaa ya wana Makambako kuwa Mbunge wao.






