Bolt yaanzisha kitufe cha dharura kwa usalama wa madereva

Special Correspondent6 years ago4 Views

Kampuni inayotoa huduma za usafiri kwa njia ya mtandaoni nchini – Bolt imezindua kitufe cha dharura (SOS)  kwa lengo la kuimarisha usalama wa madereva kipindi wanapokutana na hatari yoyote.

Akizungunza na waandishi wa  habari jana jijini Dar es Salamaam Meneja wa Bolt Tanzania Remmy Eseka alisema madereva wanaotumia programu hiyo ya Bolt sasa wanaweza kutumia huduma hiyo mpya ya usalama muda wowote watakapo hisi kuwa wapo hatarini au eneo ambalo si salama. 

Alisema matumizi hayo ya kitufe cha dharura dharura (SOS) yamekuwa kama muendelezo wa Bolt kutumia teknolojia kuimarisha usalama wa madereva wanapokuwa barabarani.

“Usalama wa dereva na abiria ni swala la muhimu sana kwetu. Tunaongeza safu ya usalama wa dereva zaidi ya ule uliopo tayari wa kufutalia mubashara safari kwa kutumia GPS na mfumo wa thathmini.

“Kitufe cha dharura (SOS) kilichopo kwenye programu ya Bolt ya dereva, huwezesha taarifa kuwafikia kampuni ya ulinzi ya SGA Tanzania Limited, kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma hizi Afrika Mashariki” alisema meneja kampuni hiyo ambayo zamani ilifahamika kwa jina la Taxify

Aidha, Meneja wa mauzo na masoko kutoka SGA, Faustina Shoo akisem kitufe cha dharura (SOS) kilichowekwa kwenye programu ya madereva kinapotumika, simu hupelekwa kwenye kituo cha dharura cha SGA, ambao baada ya kuhakiki uhalali wa dereva, wanapeleka gari la wagonjwa au timu ya askari kuelekea alipo dereva kuweza kumsaidia kama watoa huduma wa kwanza. 

“Bolt italipia gharama hizi pamoja na gharama zitakazo pitishwa kwa kila  tukio.
Tunaendeleza nia yetu ya kujibu mahitaji ya wateja/wabia kwa kutoa huduma ya uokoaji wa dharura kwa madereva wa Bolt kutokana na ubia huu. “Madereva wa Bolt wanahakikishiwa kupata huduma ya masaa 24 kupitia kitengo chetu cha dharura iwapo watapata tatizo wakiwa safarini.” alisema.

Mmoja wa abiria wanaotumia programu ya Bolt, akipata huduma kutoka kwa dereva bodaboda baada ya Bolt zamani Taxify inayotoa huduma za usafiri kwa njia ya mtandaoni nchini kuzindua kitufe cha dharura (SOS) jijini Dar es salaam jana  kwa lengo la kuimarisha usalama wa madereva kipindi wanapokutana na hatari yoyote.

 

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2vEXANx
via

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...