MSANII JACKLINE WOLPER AMSALITI KAJALA KWA WEMA SEPETU..YAANI NI MAJANGA TUPU,ONA HAPA

Admin Updates10 years ago6 Views

Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper akishoo love na Wema Sepetu.


Na Musa matejaUNAFIKI 100%!
Wakati kila mtu akiamini kwamba staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline
Wolper Massawe ni shosti wa Kajala Masanja ‘Kay’, ameibua mshangao baada
ya kunaswa akikumbatiana na Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ ambaye kwa sasa
haziivi na Kay.





TUJIUNGE KWENYE BETHIDEI
Tukio hilo lililoibua
maswali mengi yasiyokuwa na majibu ya harakaharaka lilijiri hivi
karibuni katika bethidei ya shosti wa damu wa Wema, Aunty Ezekiel
Grayson ambayo ilifanyika kwenye Mgahawa wa Rodizio, Masaki jijini Dar.


WAKUMBATIANA
Huku paparazi wetu akishuhudia na
kuwafotoa picha, Wema alipoingia tu ukumbini humo, alimkuta Wolper akila
raha zake ambapo alimkimbilia kisha akamkumbatia kwa dakika kadhaa huku
wakimwagiana mabusu kuonesha wamemaliza tofauti zao na kwamba walikuwa
‘wamemisiana’.

Wakati wamekumbatiana na kupigana mabusu walikuwa
wakinong’onezana mambo yao ambapo walipomaliza waliachia vicheko
vilivyosikika ukumbi mzima ndipo minong’ono ikaanza.


WATAALAM WA UBUYU
Kitendo cha Wema kutumia
dakika kadhaa kukumbatiana na Wolper, kilitafsiriwa na wataalam au
wafuatiliaji wa mambo ya watu (ubuyu) kuwa ni usaliti mzito kwani Wolper
ni Timu Kajala ambaye ni hasimu mkubwa wa Wema.


Wema Sepetu akimhagi Jacqueline Wolper.



“Mh! Mwenzangu makubwa, huyu Wolper si ni Timu Kajala? Inakuwaje
anatoa ushirikiano wa asilimia mia moja kwa adui wa Kajala? Hapa kuna
tatizo, unafiki kwa mastaa kamwe hauwezi kuisha,” alisikika mtoa ubuyu
mmoja aliyeomba hifadhi ya jina gazetini.


AKUMBUSHA VITA YAO
Kama hiyo haitoshi, mtoa
ubuyu huyo alikwenda mbali zaidi kwa kusema, ukiachilia mbali Wolper
kuwa karibu na Kajala lakini hata yeye (Wolper) alikuwa kwenye vita
nzito na Wema kwa kudaiwa ‘kushea’ naye penzi la msanii Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’.

“Wolper jamani mnafiki…si ndiyo huyuhuyu
aliwahi kuingia kwenye vita nzito na Wema baada ya kudaiwa kuwa
anadondoka dhambini na kipenzi cha Madam, Diamond? Yaani huu ni unafiki
asilimia mia,” alisema mtoa ubuyu huyo.


TIMU KAJALA WAJA JUU
Baada ya Timu Kajala
kusikia kwamba Wolper ‘ali-spendi’ vya kutosha na Madam kwenye bethidei
hiyo, walikuja juu kisha wakamtolea uvivu na kuanza kumshambulia katika
mitandao ya kijamii na kudai hafai kuwa timu yao.


Huku wakati huo huo… Jacqueline Wolper akishea urojo sahani moja na Kajala Masanja ‘Kay’.



“Wolper msaliti, ataendaje kwenye sherehe ya mpinzani wetu? Tena kama
hiyo haitoshi, yeye anakumbatiana na Madam ambaye kwetu sisi hatusaidii
lolote,” alisema mmoja wa Timu Kajala.


KUMBUKUMBU IPOJE?
Kabla ya siku hiyo, Wolper na
Wema hawakuwahi kuwa na uhusiano mzuri na kila sehemu ambayo utakumta
Wolper, kamwe huwezi kuona Wema ametia maguu.


WOLPER ANASEMAJE?
Baada ya paparazi wetu
kushuhudia kitendo hicho ukumbini, alimfuata Wolper na kumuuliza ni kitu
gani kilichowasababisha wapatane na kuoneshana ‘mahaba niue’ wakati
nyuma ya pazia wana bifu? Msikie alichojibu:


“Ujue watu wengi sana wamekuwa wakidhani mimi na Wema tuna bifu,
sijui kwa kuwa mimi nina ukaribu na Kajala au kwa kuwa hatujawahi kuwa
pamoja, lakini ukweli mimi na Wema siyo waongeaji sana japokuwa huwa
nikiweka picha au chochote kwenye Instagram, Wema huwa ana-like na mimi
huwa na-like vitu vyake hivyo sidhani kama nilikuwa na tatizo naye
sana,” alisema Wolper.


TUJIKUMBUSHE
Urafiki wa mastaa huwa mara nyingi
haudumu, Wema ambaye hivi sasa shosti wake mkubwa ni Aunty, kabla
aliwahi kuwa na urafiki na Snura Mushi, Jamilah wa Temba, Kajala na wote
hao akawamwaga.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.