Na Musa matejaUNAFIKI 100%!
Wakati kila mtu akiamini kwamba staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline
Wolper Massawe ni shosti wa Kajala Masanja âKayâ, ameibua mshangao baada
ya kunaswa akikumbatiana na Wema Isaac Sepetu âMadamâ ambaye kwa sasa
haziivi na Kay.
Wakati kila mtu akiamini kwamba staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline
Wolper Massawe ni shosti wa Kajala Masanja âKayâ, ameibua mshangao baada
ya kunaswa akikumbatiana na Wema Isaac Sepetu âMadamâ ambaye kwa sasa
haziivi na Kay.
TUJIUNGE KWENYE BETHIDEI
Tukio hilo lililoibua
maswali mengi yasiyokuwa na majibu ya harakaharaka lilijiri hivi
karibuni katika bethidei ya shosti wa damu wa Wema, Aunty Ezekiel
Grayson ambayo ilifanyika kwenye Mgahawa wa Rodizio, Masaki jijini Dar.
WAKUMBATIANA
Huku paparazi wetu akishuhudia na
kuwafotoa picha, Wema alipoingia tu ukumbini humo, alimkuta Wolper akila
raha zake ambapo alimkimbilia kisha akamkumbatia kwa dakika kadhaa huku
wakimwagiana mabusu kuonesha wamemaliza tofauti zao na kwamba walikuwa
âwamemisianaâ.
Wakati wamekumbatiana na kupigana mabusu walikuwa
wakinongâonezana mambo yao ambapo walipomaliza waliachia vicheko
vilivyosikika ukumbi mzima ndipo minongâono ikaanza.
WATAALAM WA UBUYU
Kitendo cha Wema kutumia
dakika kadhaa kukumbatiana na Wolper, kilitafsiriwa na wataalam au
wafuatiliaji wa mambo ya watu (ubuyu) kuwa ni usaliti mzito kwani Wolper
ni Timu Kajala ambaye ni hasimu mkubwa wa Wema.

Wema Sepetu akimhagi Jacqueline Wolper.
âMh! Mwenzangu makubwa, huyu Wolper si ni Timu Kajala? Inakuwaje
anatoa ushirikiano wa asilimia mia moja kwa adui wa Kajala? Hapa kuna
tatizo, unafiki kwa mastaa kamwe hauwezi kuisha,â alisikika mtoa ubuyu
mmoja aliyeomba hifadhi ya jina gazetini.
AKUMBUSHA VITA YAO
Kama hiyo haitoshi, mtoa
ubuyu huyo alikwenda mbali zaidi kwa kusema, ukiachilia mbali Wolper
kuwa karibu na Kajala lakini hata yeye (Wolper) alikuwa kwenye vita
nzito na Wema kwa kudaiwa âkusheaâ naye penzi la msanii Nasibu Abdul
âDiamond Platnumzâ.
âWolper jamani mnafiki…si ndiyo huyuhuyu
aliwahi kuingia kwenye vita nzito na Wema baada ya kudaiwa kuwa
anadondoka dhambini na kipenzi cha Madam, Diamond? Yaani huu ni unafiki
asilimia mia,â alisema mtoa ubuyu huyo.
TIMU KAJALA WAJA JUU
Baada ya Timu Kajala
kusikia kwamba Wolper âali-spendiâ vya kutosha na Madam kwenye bethidei
hiyo, walikuja juu kisha wakamtolea uvivu na kuanza kumshambulia katika
mitandao ya kijamii na kudai hafai kuwa timu yao.

Huku wakati huo huo… Jacqueline Wolper akishea urojo sahani moja na Kajala Masanja âKayâ.
âWolper msaliti, ataendaje kwenye sherehe ya mpinzani wetu? Tena kama
hiyo haitoshi, yeye anakumbatiana na Madam ambaye kwetu sisi hatusaidii
lolote,â alisema mmoja wa Timu Kajala.
KUMBUKUMBU IPOJE?
Kabla ya siku hiyo, Wolper na
Wema hawakuwahi kuwa na uhusiano mzuri na kila sehemu ambayo utakumta
Wolper, kamwe huwezi kuona Wema ametia maguu.
WOLPER ANASEMAJE?
Baada ya paparazi wetu
kushuhudia kitendo hicho ukumbini, alimfuata Wolper na kumuuliza ni kitu
gani kilichowasababisha wapatane na kuoneshana âmahaba niueâ wakati
nyuma ya pazia wana bifu? Msikie alichojibu:
âUjue watu wengi sana wamekuwa wakidhani mimi na Wema tuna bifu,
sijui kwa kuwa mimi nina ukaribu na Kajala au kwa kuwa hatujawahi kuwa
pamoja, lakini ukweli mimi na Wema siyo waongeaji sana japokuwa huwa
nikiweka picha au chochote kwenye Instagram, Wema huwa ana-like na mimi
huwa na-like vitu vyake hivyo sidhani kama nilikuwa na tatizo naye
sana,â alisema Wolper.
TUJIKUMBUSHE
Urafiki wa mastaa huwa mara nyingi
haudumu, Wema ambaye hivi sasa shosti wake mkubwa ni Aunty, kabla
aliwahi kuwa na urafiki na Snura Mushi, Jamilah wa Temba, Kajala na wote
hao akawamwaga.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






