Kwa mara kibao Vanessa Mdee na Jux wamekanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi licha ya kuonesha dalili nyingi ya kuwa ni item.
Lakini huenda mastaa hao wanataka
kuufanya uhusiano wao official kwa mwaka 2015. Vee Money ametoa hint
kuhusu uwezekano wa wawili hao kuwa pamoja kwenye picha aliyoweka
Instagram leo.
“A1 since Day 1,” ameandika Vanessa
kwenye picha hiyo ya black and white inayoonesha wazi kuwa wapo kwenye
dimbwi la mahaba mazito.
Naye Jux amepost picha akiwa na Vee na kuandika:
I know I’m late but better late than
never. Nataka kuwashukuru wote kwa Upendo wenu mlionyesha Mwaka wa 2014,
nawa ahidi burudani zaidi na mziki mzuri zaidi this year and hopefully
through Gods grace in the years to come. God bless your 2015. I got to
share mine with Miss Award Winner #AfricanBoy #InGodITrust.”
Akijibu swali la kama ana uhusiano wa
kimahaba na muimbaji huyo wa ‘Nitasubiri’, Vanessa aliwahi
kujibu,”Unajua labda watu hawafahamu tu lakini mie na Jux tumefahamiana
muda sana na ni mtu ambaye huwa tunashauriana hasa mambo ya kazi zetu.”
“Ni rafiki yangu wa muda sana sasa hivi.
Unajua watu wakikuona upo na mtu karibu tu lazima watasema. Mwanzo
walisema Ommy Dimpoz sababu ya ile nyimbo ya Me and You. Mara wakasema
Gosby kipindi kile ilipotoka ile nyimbo ya Monefere. Kwahiyo kwahiyo
hata leo mfano Nahareel asingekuwa na Aika basi nahisi na yeye pia
wangesema hivyo. Ila sio hivyo wanavyofikiria. Jux ni rafiki yangu tu,”
Vee aliiambia Bongo5.
Naye Jux alikuwa na majibu yale yale
pindi swali hilo lilipokuwa likitupwa kwake. “No ni mshikhaji wangu tu,
tunafanya naye kazi, kuna tabia zinaendana, kama ninavyokuwa na rafiki
na Stamina, Mo Music ni kawaida, sema unajua ni mwanamke na ni njia
toafuti ndio maana imekuwa hivyo,” alisema Jux.
Hata hivyo alipoulizwa kama Vanessa anafaa kuwa wife material Jux alijibu Vanessa ana kila sifa ya kuwa mke.
“Ni msichana mzuri, mwonekano wake
mzuri, she is smart, yeah she is a wife material, yuko vizuri, lakini na
mimi tumeendana sana tabia zetu kama washikaji. Sema nipo naye karibu
na kwa sababu mimi sionekanagi na wasichana wengi ndio maana imekuwa
hivyo. Lakini sijui labda baadaye kwa sasa hivi ni mapema, vyote
anapanga Mungu,” alisisitiza Jux.