Kwa mujibu wa chanzo cha GPL , kwa kipindi kirefu, Snura amekuwa
akionekana nyakati za usiku akiwa na mume wa Davina, wakati mwingine
mwanaume huyo anaenda nyumbani kwa Snura au wawili hao kuzungumza kwa
muda mrefu ndani ya gari la mwanaume huyo.
“Yaani mastaa wa Bongo bwana, wanapenda sana kuchukuliana mabwana. Huyu
Snura anatoka na mume wa mwenzake. Mume wa Davina huwa anakuja nyumbani
kwa Snura mara kwa mara hasa nyakati za usiku.
“Wakati mwingine anakuja na gari na kupaki jirani na nyumbani kwa Snura
kisha wanakaa kwenye gari kwa saa kibao. Snura anamzunguka rafiki yake,
fuatilieni mtaujua ukweli,” kilisema chanzo chetu.
Baada ya kuunyaka ubuyu huo, GPL iliamua kuingia mzigoni kwa kumsaka
Snura na alipopatikana, akasomewa tuhuma zake ambapo katika hali ya
kushangaza, msanii huyo, alimwaga chozi.
Alipomaliza kulia, Snura alianza kufunguka ukweli wa kisa hicho ambapo
alikiri kuwa ni kweli mume wa Davina alikuwa akienda nyumbani kwake mara
kwa mara lakini ilikuwa ni kipindi ambacho Davina na mwanaume huyo
walikuwa wametibuana kiasi cha msanii huyo kufungasha virago vyake na
kutokomea kusikojulikana.
“Mimi nilikuwa nahangaika kuwapatanisha kwa sababu walikuwa kwenye
mgogoro mkubwa, mumewe akawa ananiomba nimsaidie kumbembeleza Davina
arudi wayazungumze na kumaliza matatizo yao ili kuokoa ndoa yao
isivunjike.
Davina nae alitafutwa ili kujua kwa upande wake analizungumziaje sakata hilo ambapo msanii huyo alitema nyongo. Hebu msikie:
“Watu wengine hawana kabisa kazi za kufanya, yaani walikuwa wanataka
kunigombanisha na shosti wangu lakini wameshindwa. Ni kweli na mimi
niliwahi kuletewa taarifa kwamba mume wangu anaonekana nyumbani kwa
Snura usiku lakini ilikuwa ni kipindi ambacho nilikuwa kwenye matatizo
na mume wangu.
“Kiukweli Snura hawezi kufanya hivyo kwa sababu yeye ndiye aliyepigania
ndoa yangu isivunjike. Isitoshe sisi tunaishi kama ndugu, watoto wangu
huwa wanaenda kushinda kwake na wakati mwingine huwa namtuma mume wangu
akawachukue kwa hiyo hata kama wanamuona kwake, siyo kwa nia mbaya, watu
aache uchonganishi,” alisema Davina.