PENZI MATATA LA NAY, SHAMSA: MUME WA SHAMSA , SIWEMA VIILIO
Ney na Shamsa wakifuatilia jambo kwenye simu.Musa mateja na imelda mtema
Penzi
matata linalowanyima usingizi baadhi ya watu mjini kwa sasa kati ya
mwigizaji wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford na mkali wa Bongo Fleva,
Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ limeibua tafrani kubwa huku waliokuwa
wapenzi wa mastaa hao wakijikuta wakiangua vilio kweupe, Ijumaa
limesheheni.
Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego na Shamsa Ford wakipozi kimahaba. TATIZO MAHABA NIUE
Mara
baada ya wawili hao kutangazwa rasmi kuwa sasa ni mahaba niue huku
picha za ushahidi zikimwagwa, aliyekuwa mwandani wa Nay, Siwema a.k.a
Wemalicious na aliyekuwa mume wa Shamsa, Dickson ‘Dick’ wanadaiwa
kujikuta kwenye hali mbaya kiasi cha kumwaga machozi.
TUJIUNGE NA CHANZO KWA SIWEMA
Habari
kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa Siwema jijini
Mwanza zilidai kwamba, mara baada ya picha za wawili hao kuzagaa kwenye
mitandao ya kijamii aliumia roho hasa alipomuona Shamsa akijiachia
kwenye nyumba ambayo alishirikiana na Nay kuijenga.
“Yaani Siwema
ameumia hadi akajikuta akiangua kilio kwa uchungu. Sikukuu ya Pasaka
ilikuwa mbaya kupita kiasi kwa Siwema. “Kinachomuuma zaidi ni kwamba
hata nguo zake za mtoko Shamsa anavaa ‘gym’ na kufanyia mazoezi. Jamani
kuna dharau zaidi ya hiyo? “Ukweli roho inamuuma vibaya mno,” kilisema
chanzo hicho kwa ombi la kutochorwa jina gazetini.
Kabla ya kuhamia
kwa chanzo cha mume wa Shamsa ili kupata ubuyu kamili, gazeti hili
lilimsaka Siwema ili kujua anachukuliaje jambo hilo ambapo alifunguka ya
moyoni.
SIWEMA AANIKA MAZITO
Akizungumza na Ijumaa kwa njia ya
simu kutoka jijini Mwanza, Siwema mwenye mvuto wa kuvunja midume shingo
alianika mazito kwamba, kitendo cha Nay kumuacha na muda si mrefu kwenda
kwa Shamsa ni upuuzi.
Siwema alifunguka kwamba, kinachomshangaza ni kitendo cha Shamsa kuvaa nguo zake na kufanyia mazoezi.
Mwanamama huyo alisema watu watamtukana kwa kuwa hawajui tabia ya Nay kwani hata Shamsa atamshindwa tu.
“Nilivumilia vitu vingi sana. Maumivu nayajua mimi, nyumba tuliyojenga
wote, anaingia mwanamke mwingine. Namhurumia sana Shamsa kwani hajui
tabia za Nay,” alifunguka mtoto mweupe, Siwema kwa uchungu.
KUMBE SIWEMA ALIJUA
Habari
zilieleza kwamba, Siwema alijua muda mrefu kuwa Nay anatembea na Shamsa
lakini alipomuuliza staa huyo anayetamba na Ngoma ya Akadumba
alimwambia walishaachana.
Siwema. NAY ANASEMAJE?
Akizungumzia ishu hiyo, Nay alisema kuwa yeye yupo na Shamsa na kwamba anamshangaa huyo Siwema kwani alishaachana naye.
TUJIUNGE NA CHANZO KWA MUME WA SHAMSA
Kwa
mujibu wa chanzo makini, naye kama Siwema, baada ya penzi la Shamsa na
Nay kuwa ndiyo habari ya mjini huku wakitupia picha za malovee
mtandaoni, mume wa Shamsa, Dick alipaniki kiasi cha kutokwa machozi huku
akitafuta namna ya kupooza machungu.
JB AOMBWA AOKOE JAHAZI
Habari
zilidai kwamba, Dick alikimbilia kwa staa wa sinema za Kibongo, Jacob
Steven ‘JB’ na kwenda kumuomba aokoe jahazi akimshitakia Shamsa kuwa
ameamua kumwacha na kuamua kutembea na Nay, jambo ambalo analiona kuwa
ni udhalilishaji kwani ni mkewe ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume,
Terry.
Mwanamuziki
kinara wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Ilidaiwa kuwa,
baada ya Dick kufika nyumbani kwa JB maeneo ya Ubungo-Kibangu, Dar na
kumweleza hayo, mwigizaji huyo alimpigia simu Shamsa ambaye humwita
Daddy na kumuuliza juu ya suala hilo ambapo alimweleza kuwa alishaachana
na Dick hivyo kila mmoja ana maisha yake.
Katika hali hiyo, JB aliwataka kukaa chini na kuyamaliza kiutu uzima kuliko kuwekeana kinyongo.
SHAMSA ANASEMAJE?
Baada
ya kusikia kilichopo upande wa mume wa Shamsa, gazeti hili lilimgeukia
Shamsa na kumwelezea kila kitu kilichopo ambapo alionesha kumshangaa
Dick kwa kuwa alishamalizana naye tangu Oktoba, mwaka jana.
“Kwanza
namshangaa kwa nini anawaka wakati kila mtu ana maisha
yake?“Tulishaachana tangu mwaka jana so kila mtu ana maisha yake,”
alisema Shamsa ambaye kwa sasa amehamishia moyo wake kwa Nay.
Aliyekuwa mume wa Shamsa, Dickson ‘Dick’. DIAMOND ACHAFUA HALI YA HEWA
Wakati
sakata la Shamsa na Nay likishika kasi mithili ya moto wa kifuu,
mwanamuziki kinara wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
amechafua hali ya hewa baada ya kutundika mtandaoni picha ya mahaba ya
wapenzi hao iliyosababisha tafrani zaidi.
Diamond ambaye ni
swahiba wa Nay ndiye aliyekuwa wa kwanza kuweka picha iliyomuonesha Nay
‘akibusiana’ na Shamsa kupitia ukurasa wake wa Instagram hivyo
kuwapandisha hasira Siwema na Dick kwani alionekana kufurahishwa na
‘pea’
0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)
Stay Informed With the Latest & Most Important News