Baba
mzazi wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul
Jumaa ‘Baba D’.Baba D alitiririka kwamba mastaa hao wa kike ambao Mbongo
Fleva huyo aliwahi kutoka nao huenda wao ndiyo hawana kizazi hivyo
wanamtupia lawama mtoto wake kwa kushindwa kuwazalisha.
Alisema kuwa
kikubwa anachokiamini wote hawakuwa na upendo wa kweli kwa mwanaye,
walitaka kuzitumia tu fedha zake na kumuacha solemba lakini sasa Zari
ndiye mwenye penzi la dhati kwa mwanaye.
“Kiukweli Zari kanifurahisha. Ndiye mkwe wangu wa kweli na halali kabisa.
“Nampongeza sana Zari kwa kushika ujauzito wa mwanangu. Sasa Diamond atatembea kifua mbele kwa kujiamini,” alisema baba D.
Alisema
kutokana na kile kilichokuwa kikiaminika kuwa hana maelewano mazuri na
mkali huyo wa Bongo Fleva, kwa sasa wapo vizuri na hata akiwa na tatizo
huwa anamwambia Diamond ambaye amekuwa akimpa msaada.
“Kwa sasa nina
maelewano mazuri na Diamond, muda wowote nikiwa na tatizo huwa
namjulisha ananisaidia, kitu ambacho kinamfanya amgharamie mama yake
kuliko mimi ni kwa sababu aliishi naye kwa kipindi kirefu na kuhangaika
naye tangu utotoni,” alisema.
Ukiacha Zari ambaye amekubali kubeba
ujauzito wake, Diamond aliwahi kuwalalamikia baadhi ya wapenzi wake kuwa
walikataa kumzalia mtoto akiwemo Wema, Penny na Jokate Mwegelo