Tetesi za Usajili Tanzania Leo
Kila kitu kipo tayari mlindamlango wa Simba SC Aishi Manula atajiunga Azam FC dirisha kubwa ambayo ndiyo timu iiyomtambulisha kwenye ramani ya mpira wa miguu.
Beki Lameck Lawi (19) ataondoka Coastal Union mwishoni mwa msimu huu. Mkataba wake na Coastal unamalizika na atakuwa mchezaji huru.
Kuna uwezekano mkubwa Orlando Pirates wakamtoa kwa mkopo tena kiungo Mshambuliaji Deivi Miguel Viera, Gilberto(24) kwenda timu Ile Ile Petro De Luanda msimu ujao, Singida BS ni miongoni mwa timu zilizo ulizia uwezekano wa kupata huduma ya mchezaji huyo.
Klabu ya Yanga Sc imevutiwa na huduma ya mshambuliaji JephteKitambala Bola ambaye amefunga jumla ya magoli 10 msimu huu akiwa na klabu ya AS MANIEMA.
Hakuna OFA iliyowasilishwa lakini jina lake ni miongoni mwa majina yaliyopo kwenye list ya washambuliaji wanaotazamiwa kusajiliwa .
Klabu ya Simba sc wanavutiwa na huduma ya kiungo mshambuliaji Basoala Agee kutoka nchini congo ndani ya klabu ya AS Maniema. Mchezaji huyo ana uwezo wa kucheza kama winga, mshambuliaji pamoja na kiungo mshambuliaji amezivutia klabu nyingi ikiwemo kaizer chiefs,Yanga Sc pamoja na Simba sc.
Hakuna OFA iliyowasilishwa zaidi ya kuulizia huduma yake na wanaendelea kufwatilia maendeleo yake ndani ya klabu hiyo.
Rulani mokwena ameonyesha utayari wa kujiunga na klabu ya Orlando pirates kama wakiwa tayari kuhitaji huduma yake, Kocha huyo pia anawinda na Yanga ya Tanzania.
Azam FC wanakaribia kumsainisha mshambuliaji wa SC Villa Charles Lwanga “Neymar”(25). Wameshakubaliana Kila kitu na mchezaji kilichobaki ni vilabu kukamilisha mazungumzo na kumalizana.
Simba SC wameulizia upatikanaji wa kiungo raia wa Mali Lassine Kouma(21) anayeichezea Stade Malien kwa sasa.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






