Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kongamano utamaduni katika ya China Tanzania pamoja na uzinduzi wa kinywaji cha Pombe Kweichow Moutai litakalofanyika Mei 9 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam Mwakilishi wa Kampuni ya China Moutai Group Charles Wang amesema kuwa ujio wa kinjwaji hicho ni kufungua fursa kati ya nchi ya Tanzania na China ambapo biashara ya kiywaji hicho kuingia Tanzania inakuwa nchi ya pili kwa Afrika.
Amesema kuwa kinywaji hicho ni maarufu kwa nchini China hivyo soko la Tanzania ni kudumisha mikakati ya kukuza ushirikiano wa kibiashara baina ya mataifa nje ujulikanao Belt Road Initiative.
Wang amesema katika uzinduzi huo viongozi mbalimbali watahudhuria wa serikali na wanadiplomasia ,wafanyabiashara kutoka China pia na ujumbe wa maofisa wa kampuni hiyo wataongozwa na Makamu Katibu Mkuu wa Chama ambaye ni Mkurugenzi wa Bodi ya Kampuni.
Amesema kuwa mara ya kwanza kinywaji hicho kiliingia Afrika Kusini mwaka jana hivyo imeendelea kupanua soko latika nchi za Afrika na kuwa wazalishaji wa bidhaa zenye ubora ambazo zinatamba katika masoko mbalimbali ya Kimataifa Duniani.
Mwakilishi wa China Moutai Group Charles Wang akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ujio wa kinywaji cha Pombe cha Kweichow Moutai nchini katika uzinduzi utaofanyika Mei 9 jijini Dar es Salaam.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2PQRuD1
via