Ronaldo Apata Kombe kwa Mara ya Kwanza Juve, Mayweather Ampongeza

Special Correspondent6 years ago7 Views

Ronaldo Apata Kombe kwa Mara ya Kwanza Juve, Maywether Ampongeza

BONDIA mstaafu Floyd Mayweather, juzi alipata nafasi ya kukutana na mastaa wa Juventus wakiongozwa na Cristiano Ronaldo baada ya timu hiyo kuifunga AC Milan na kubeba kombe la Super Cup.

Bondia, 41, huyo alikaribishwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya Juventus kushinda bao 1-0 mfungaji akiwa ni Ronaldo katika mchezo uliopigwa Saudi Arabia ambapo pia ni kombe la kwanza la Mreno huyo tangu atue hapo akitokea Real Madrid, mwanzoni mwa msimu huu.

Mbali na kusalimiana na wachezaji kadhaa wa timu hiyo, alipata nafasi ya kupiga picha na kombe hilo. Wachezaji wengine aliopiga nao picha ni Paulo Dybala, Giorgio Chiellini na Blaise Matuidi. Katika mchezo huo, Ronaldo, 33, alifunga bao katika dakika ya 61 akimalizia krosi ya Miralem Pjanic, likiwa ni bao lake la 16 msimu huu

from UDAKU SPECIAL BLOG http://bit.ly/2FyR5mi
via

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...