PICHAZ: KAJALA AJITOA FAHAMU….AFANYA SASAMBU YA KUFA MTU BAADA YA KULEWA CHAKARI

Admin Updates10 years ago7 Views

CHIZIKA! Katika
hali ambayo haikutarajiwa, staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja
amewaacha watu midomo wazi kwa kukatika mauno hadharani.

Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja akikata mauno.
Tukio
hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni maeneo ya Twende Polepole,
Mkoa wa Pwani kwenye sherehe ya kumkaribisha mtoto wa mwigizaji Aunt
Ezekiel (Baby Shower) iliyohudhuriwa na watu wengi akiwemo Kajala.
Awali,
mwanahabari wetu aliyekuwa akikusanya matukio eneo hilo alimshuhudia
Kajala akipata ‘kilaji’ kisha akaitwa na mshereheshaji Maimartha Jesse
na kupewa nafasi ya kucheza muziki ndipo alipoanza kuionesha tatuu yake
iliyopo bajani kabla ya kuanza kukata mauno.


…akizidi kunengua.
Watu
waliokuwepo ukumbini humo walipigwa na mshangao kwani hakuna aliyeamini
staa kama huyo alikuwa mahiri wa kuzungusha nyonga.“Yaani
ni balaa, sijui ni kuzidisha kilaji au ni vipi, mtoto wa kike kajitoa
ufahamu kwelikweli, leo ndiyo amefunika watu wote hapa,
” alisema mmoja wa waalikwa.
“Aunt
Ezekiel kwa kushirikiana na marafiki zake, waliamua kufanya sherehe kwa
lengo la kufurahi pamoja na kumpa mwigizaji huyo zawadi mbalimbali za
mtoto wake mtarajiwa.
Mbali
na Kajala, sherehe hiyo ilihudhuriwa na mastaa kadhaa akiwemo Husna Idd
‘Sajenti’ (mwigizaji), Nice Chande (muigizaji), Zamaradi Mketema
(mtangazaji) na wengineo ambao nao walicheza muziki, kula na kunywa.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...