Kanali Ndayalina ameyasema hayo kwenye ukumbi wa NSSF uliopo Manispaa ya Kigoma mjini kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari.
Mkuu wa Wilaya huyo ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga kama mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo alisema kuwa wanahabari wana nafasi kubwa ya kuchochea kukua kwa uchumi wa Taifa iwapo watatumia vizuri nafasi zao.
“Nyie wanahabari ni kiungo kizuri kati ya jamii na serikali yao endapo mtatumia vizuri kalamu kuelimisha jamii mambo mbalimbali ya kuchochea maendeleo uchumi wa Taifa letu utapanda”Alisema
Pia amewataka wanahabari kuandika habari zao kwa usahihi kama sheria inavyowaelekeza hasa katika kipindi hiki tunachoelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika octoba mwaka huu.
Naye Rais wa umoja wa muungano wa vilabu vya waandishi Tanzania(UTPC)Deogratius Nsokolo lengo kubwa ni kuona waandishi wanafuata maadili ya kazi za uandishi na kuwataka waandishi wa habari nchini kuwa sehemu ya mabadiliko hasa kwenye kipindi hiki kinachoelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2020.
Baadhi ya wadau wa habari waliohudhuria katika maadhimisho hayo wamewataka wadau kutoa ushirikiano kwa waandishi ili habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2DOHYvt
via