MBUNGE MALEMBEKA AHAMASISHA WATANZANIA KUPENDA KWENDA HIFADHI ZA UTALII

Special Correspondent6 years ago5 Views


Na Heri Shaban,Dodoma 

MWENYEKITI wa Taasisi ya Utalii 255  ambaye pia ni   Mbunge wa Mkoa wa kaskazini Unguja Angelina Malembeka  ,amewahamasisha Watanzania  kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi za Mbunga za Utalii, zilizopo nchini ili  kujifunza utalii wa ndani na kuona vivutio vilivyopo.

Mbunge Malembeka aliyasema hayo Bungeni Dodoma leo  wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada kupokea wageni wake ,Wahamasishaji wa Kundi la Utalii 255 kutoka Tanzania Bara leo walishiriki kusikiliza kikao cha maswali na majibu Bungeni Dodoma.

Alisema ziara ya Wahamasishaji wa Utalii wa 255 Kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar wapo katika ziara ya siku tatu ,wameanza kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kesho Mei 4 ziara inaelekea kutembelea Mbuga ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangile Mkoa wa Mnyara.

“Hii ni sehemu ya  kampeni ya kutangaza Utalii wa ndani ,kundi la Utalii 255 linawataka Watanzania kuweka mazoea ya kutembelea hifadhi za Taifa kuangalia mambo mbalimbali  ikiwemo wanyama kama sehemu ya kujifunza”alisema Malembeka

Alisema Utalii 255 ilianzishwa hivi karibuni,ikiwa na lengo la kuwahamasisha na kuwakumbusha Watanzania kuweza kujiwekea utaratibu wa kutembelea Hifadhi na Vivutio vya Utalii vilivyopo Nchini, Ziara hii imewashirikishaka Vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar. 

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2ZZMKj1
via

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...