MASKINI ANGELINA JOLIE! BAADA YA KUKATWA TITI, SASA AFANYIWA UPASUAJI, ATOLEWA OVARI, MIRIJA YA UZAZI
Angelina
Jolie.MWIGIZAJI wa filamu nchini Marekani, Angelina Jolie amelazimika
kutoa ovari zake pamoja na mirija ya uzazi baada ya uchunguzi kuonesha
kuwa alikuwa katika hatari ya kuathirika na saratani ya nyumba ya uzazi.
Angelina
Jolie, mumewe Brad Pitt wakiwa na watoto wao.Staa huyo maarufu wa
Hollywood amelidokezea jarida la New York Times, kuwa alilazimika kutoa
viungo hivyo wiki iliyopita katika upasuaji wa dharura.
“Upasuaji huo
ulitokana na ripoti ya uchunguzi wa daktari uliobaini kuwa nilikuwa na
asilimia 50 ya chembechembe zenye hatari ya kuambukizwa saratani”
alisema Jolie
Habari hizi zimewashtua mashabiki wa mrembo huyo
ambaye miaka miwili iliyopita alilazimika kukatwa titi kwa sababu ya
tishio hilo hilo la Saratani.
Angelina
Jolie akiwa na mumewe Brad Pitt.Mama mzazi wa staa huyo aliaga dunia
kufuatia hitilafu iliyotokana na matibabu ya saratani.
“Siyo jambo rahisi sana kukabiliana na swala hili gumu linalohusu afya yangu” aliongeza Jolie.
Jolie
ambaye ni mke wa mwigizaji nyota wa Holywood, Brad Pitt, anasema kuwa
vipimo vilionesha chembechembe za maradhi hayo na ikamlazimu kuchukua
hatua hiyo mara moja.
Mastaa hao wana watoto sita ambapo kati yao wengine ni wakuhasili.
0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)
Stay Informed With the Latest & Most Important News