
Mkuu wa Gereza la Shinyanga Paulo sabuni Kamole (kulia) akipokea msaada wa sabuni za kufulia na kuogea pamoja na dawa za meno kutoka kwa Ofisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga Lidya Kwezigabo.
Mkuu wa Gereza la Shinyanga Paulo Sabuni Kamole, akishukuru msaada huo kutoka kwa Maofisa Ustawi wa Jamii kwa ajili ya kuwatatulia changamoto ndogo ndogo wafungwa wanawake pamoja na kuwapatia elimu ya ulinzi wa mtoto.
Ofisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga Lidya Kwezigabo akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Chamaguha na kuwataka wapinge masuala ya ukatili ndani ya jamii kwa kuanza na wao wenyewe.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Chamaguha Shinyanga mjini wakisikiliza kwa makini elimu ya makuzi na kupinga masuala ya ukatili ambayo yamekuwa yakizima ndoto zao.
Wanafunzi wakiendelea kusikiliza elimu ya kupinga ukatili.
Ofisa ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Elizabeth Mweyo, akiwataka wanafunzi hao hasa wa kike waache kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi wakiwa katika umri mdogo na kuacha tamaa ya kupenda chips na Lift, ili wapate kutimiza ndoto zao.
Ofisa ustawi wa jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini Agnes Cinethon akiwataka wanafunzi hao hasa wa kike pale wanapobakwa wawahi kwenye vituo vya afya ili waweze kupatiwa matibabu ya haraka na kuwazuia kutopatwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
Ofisa ustawi wa jamii mkoa wa Shinyanga Sophia Kang’ombe ambaye huwa ana hudumia Kambi ya wazee Kolandoto akiwataka wanafunzi hao kupenda Babu na Bibi zao wakiwamo na wazazi ili kujenga mahusiano mazuri ambayo yatawasaidia kuwa wanatatuliwa shida zao, ikiwamo na kutoa taarifa za watu kutaka kuwafanyia ukatili na kuweza kutatuliwa.
Wanafunzi wakiendelea na upewaji wa elimu ya makuzi na ukatili.
Mwanafunzi Naomi Geogre akiuliza swali namna kesi za ukatili zitakavyoshughulikiwa pale watakapokuwa wakitoa taarifa za matukio hayo.
Mwalimu mkuu msaidizi wa Shule ya Sekondari Chamaguha Abdalla Lidyati, akielezea kufurahishwa na ujio wa mofisa ustawi kwenye shule hiyo na kutoa elimu ya makuzi na ukatili, hali ambayo itasaidia kusiwepo na mimba shuleni hapo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ushirika nao wakisikiliza elimu ya ukatili na kutakiwa wawe wanatoa taarifa mapema pale wanapoona kutaka kufanyiwa vitendo hivyo, ili vipate kushughulikiwa kabla ya kuwaletea madhara.
Ofisa Ustawi wa Jamii wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Elizabeth Mweyo akitoa elimu ya kupinga ukatili kwa wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika. . Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blogfrom MICHUZI BLOG https://ift.tt/2WcQOK8
via






