MALI ZA WAKILI MIKONONI MWA SERIKALI,HAKIMU WAKILI KUPANDISWA MAHAKAMANI

Special Correspondent6 years ago5 Views

Na Ahmed Mahmoud,Arusha

Serikali imetaifisha rasmi Mali za Wakili maarufu Nchini Median Mwale zenye thamani ya sh,bilioni 1.2 zilizotokana na zao la utakatishaji mara baada ya mahakama kuu kumtia hatiani na kuamuru Mali hizo zitaifishwe.
Akiongea na wandishi wa habari jijini Arusha,katika zoezi la makabidhiano ya mali hizo kati ya ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka DPP na Hazina,Mkurugenzi wa Mashtaka ya jinai Nchini , (ASP )Biswalo Mganga alizitaja Mali hizo kuwa ni pamoja na Magari sita ya kifahari yanayoshikiliwa kituo kikuu cha polisi,jijini hapa.

Mali zingine zilizotaifishwa ni pamoja na Nyumba mbili ikiwemo iliyopo ploti Namba 261 block c Njiro na nyumba nyingine iliyopo ploti namba 22 iliyopo eneo la Ilikyurei ambayo ilikuwa mali ya Wakili Loomo Ojale na shamba moja la ekari 10 lililopo eneo la Ngaramtoni.

Alisema hatua hiyo imekuja kufuatia mahakama kuu kanda ya Arusha,kutaifisha Mali hizo na kwamba April 14,2019 mahakama hiyo ilitoa kibali cha kuzitaifisha rasimi na kuwa Mali ya serikali.

“Kwa mujibu wa sheria Mali zinapotaifishwa kuwa Mali ya serikali zinakuwa chini ya katibu mkuu Hazina” Alisema.

Naye kaimu mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa Mali za serikali Hazina,Benezeth Rutta Alisema kuwa Mali hizo baada ya kukabidhiwa kutoka kwa DPP zinakuwa chini ya uangalizi wa wizara ya fedha zinapangwa kadri serikali itakavyoona inafaa.

“Mali hizi Mara baada ya kukabidhiwa serikalini zitapangiwa matumizi kadri serikali itakavyoona inafaa na kama itaonekana Mali hizo hazifai kwa matumizi ya serikali zitauzwa kwa mnada” Alisema Rutha.

Kwa upande wake kamishina msaidizi wa jeshi la Polisi ,Selemani Nyakulinga Alisema Alisema kuwa mwaka 2011 alipata taarifa kutoka kitengo cha udhibiti wa fedha haramu kuwa kuna watu waligushi na kutaka kuiba fedha dolla la marekani milioni 17.2 kutoka mfuko wa global fund kwa ajili ya kusaidia kutibu malaria na HIV Nchini Tanzania zikitoka kwenye Hazina ya nchi ya Marekani.

Alisema walibaini kuwa waliohusika na wizi huo ni RAIA wa Kenya wakishirikiana na watanzania akiwemo Wakili Median Mwale .

Alisema baada ya kufuatilia walifanikiwa kuwatia mbaroni wahusika wote na baadae mahakama ilibaini kuwa wahusika walishanunua Mali mbalimbali zilizotokana na zao la utakatishaji wa fedha hizo na mahakama kuridhia na kutaifisha Mali hizo kuwa za serikali.

“Leo tulikuwa tumekuwa kuwaonyesha na kuwakabidhi rasimu kuwa wamiliki wapya wa Mali hizo”Alisema Nyakulinga.

Wakati huo huo DPP Biswalo Mganga amesema Wakili Maneno Mbunda na watuhumiwa wengine tisa wanashikiliwa kwa mahojiano kwa makosa mbalimbali .
Biswalo amesema Mtuhumiwa huyo ambaye pia ni Mtumishi wa Serikali katika Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Hakimu ambaye hakutajwa Jina lake, walishirikiana kufanya Kosa la kuhujumu Uchumi kwa kutamka Bei ya chini ya Meno ya Tembo na kumuachia huru Mtuhumiwa.

Tuendelee kushikamana na kupaza Sauti pale wenzetu wanapokumbwa na masahibu ya aina hii maana Nchi hii sasa ilipofikia sio sawa kabisa. Ukitekwa na watekaji wasisikie kelele huku nyuma yao ni rahisi sana kufanya yao.

Tuondoe hofu na uoga ili tuwe na udhubutu kama sio utayari wa kuwatetea na kuwapigania wenzetu. Ukiwa na hofu huwezi kusema, na usipoanza kusema wewe, Siku nawe yakikusibu, hutopata Watu wa kukusemea.

Awali Wakili Mbuda ilidaiwa alitekwa na watu wasiojulikana na taarifa za kutoweka kwake ziliendelea kuenea kwa kasi jijini hapa na hakuna chombo chochote cha doka kilichokuwa tayari kulizungumzia suala hilo

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2J4e2Qe
via

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...