
Halima Bulembo,Jesca Magufuli na wengine wanne wachaguliwa UBUNGE Viti Maalum UVCCM
Msimamizi wa uchaguzi wa Viti Maalum kupitia kundi la UVCCM Bara na Zanzibar watakaowakilisha Vijana kwenye Bunge la Tanzania, leo asubuhi ya August 2 2025, ametangaza matokeo ya kura zilizopigwa usiku wa kuamkia leo ambapo kwa Tanzania Bara wamepatikana Wagombea sita.
Jumla ya Wagombea walikuwa ni 48 (Tanzania Bara 31 na Zanzibar 17) na Wagombea hao 10 (sita wa Bara na wanne wa Zanzibar ) ndio walioshinda baada ya kupata kura za juu zaidi kuliko wengine ambapo kwa upande wa kura zilizopigwa Tanzania Bara jumla ni kura 2466 (Kura zilizoharibika ni 12 na kura halali 2454), na Zanzibar zimepigwa kura 1652 (zimeharibika kura 8 na kura halali 1644)






