Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa awasihi wafungwa 73 waliohitimu mafunzo ya ufundi standi kutoka magereza mbalimbali nchini kuutumia ujuzi walioupata kwenye mafunzo hayo uweze kuwanufaisha kiuchumi muda ambao adbabu zao zitakapomalizika. Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe, Malisa amesema lengo la Serikali chini ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuwapa ujuzi wafungwa kubadilisha maisha yao na kuisambaza elimu walioipata kwa wafungwa wengine na kuwakumbusha kuzitumia vizuri Halmashauri kuhakikisha kuwa moja ya kundi linalopata fursa ni pamoja na kundi hilo.
Aidha Mhe. Malisa ameishukuru Serikali kwa kuhakikisha inarasimisha fani mbalimbali ambazo zimetoka katika taaasisi zisizo rasmi na kuzirasimisha ili kwenda kwenye soko la ajira na kwenda kujiajiri.