Atakayekamatwa anakata mti hovyo Sukuma Ndani-RC Mwanri

Special Correspondent6 years ago5 Views

Na Editha Edward-Michuzi TV Tabora 
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ametoa onyo kwa mtu atakaye haribu mazingira kwa njia ya ukataji wa miti hovyo.
Kauli hiyo ameisema wakati akishiriki zoezi la upandaji wa miti na wanafunzi wa chuo cha Teknolojia cha Dar es Salaam (D. I. T) katika kata ya kanyenye manispaa ya Tabora ikiwa ni juhudi za kuboresha Mazingira 
“Mtu atakayekamatwa anafanya Uharibifu wa Mazingira atasukumwa ndani, tunachofanya hapa ni kuotesha miti kila Halmashauri iwe na vitalu vyake kuanzia kwa mkuu wa Mkoa, mkuu wa Wilaya mtendaji wa kata, Mtendaji wa kijiji pamoja na Mtendaji wa mtaa, tunataka tuhakikishe miti hii inapandwa katika Taasisi zote”Amesema Mwanri
Aidha kiongozi wa Wanafunzi wa Chuo cha D. I. T Machage Emmanuel amesema Lengo la kushiriki zoezi hilo la upandaji wa miti ni kuimarisha Mazingira na kupata uhifadhi wa vyanzo vya maji na kuifanya Tabora kuwa ya kijani.
Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ambaye ameshiriki zoezi la upandaji wa miti pamoja na wanafunzi wa chuo cha D. I. T.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2WykySb
via

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...