

Video zimeonesha ndege hiyo ya Sukhoi Superet -100 ilipata hitilafu na kulazimika kutua kwa dharura huku sehemu za ndege hiyo ikiwaka moto katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo Moscow.
Baadhi ya picha za video zimeonesha baadhi ya abiria wakiruka kutoka katika sehemu zilizokuwa zinawaka na kuruka katika nyasi na sehemu salama.
Imeelezwa kuwa watoto wawili ni moja kati ya watu waliopoteza maisha na tayari wapelelezi kutoka Urusi wameshaanza kufanya uchunguzi kufuatia tukio hilo.
Waziri wa Afya wa Moscow Dmitry Matveyev amesema kuwa katika ajali hiyo watu 11 wamejeruhiwa, na watatu kati yao wameruhusiwa kutoka hospitali na hali zao zinaendelea vizuri.
Mamlaka ya uwanja wa ndege Moscow Urusi umesema kuwa ndege hiyo ilitua kwa dharura baada ya tatizo la kiufundi kutokea ikiwa angani na wachunguzi watafanya utafiti kupitia mashahidi, wahanga pamoja na wafanyakazi wa ndege wa la shirika hilo.
Ndege hiyo ya Sukhoi aircraft ilikuwa inaruka kutoka Moscow kuelekea mji wa kaskazini wa Urusi (Murmansk) kabla ya kurudi uwanjani na ilibeba abiria 73 na wafanyakazi wa ndege 4.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2PLueX9
via






