- Home
-
- P-SQUARE WAMUUMBUA DIAMOND PLATNAM..!! HAYA NDIYO WALIYOSEMA
P-SQUARE WAMUUMBUA DIAMOND PLATNAM..!! HAYA NDIYO WALIYOSEMA

Mwanamuziki wa P square, Peter Okoye
ameoneshwa kushangazwa na taarifa kwamba mwanamuziki wa bongo fleva
Naseeb Abdul alihudhuria harusi yake hivi karibuni nchini Nigeria na
kuhudhuriwa na mastaa mbali mbali akiwenmo msukuma gozi wa Totenham
Hotspurs Adebayor.
Awali kupitia blogs mbali mbali
kulisambaa taarifa kuwa dimond alikua mwanamuziki pekee afrika mashariki
aliyealikwa katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na tajiri nambari moja
afrika, Aliko Dangote.
Blogs hizo zilikwenda mbali kwa kumpamba
diamond kwa vyeo vya ajabu ajabu ikiwemo Michael Jackson wa afrika
mashariki jambo ambalo lilisababisha wengi kumponda.
Akihojiwa na kituo cha EATV mara baada
ya kuwasili jijini Dar kwa ajili ya shoo iliyopigwa viwanja vya leaders
club, Okoye alishangazwa na taarifa za dimond kuhudhuria katika harusi
yake.
Okoye alikua akijibu swali aliloulizwaa
na mtangazaji wa kipindi cha HotMix Adrian Hilary kuhusu diamond
kuhudhuria harusi hiyo ambapo alionesha kushangazwa na jina hilo na
kuhoji Diamond ni nani?
Kushangaa huko kulimaanisha licha
Diamond kujichezesha mbele ya Okoye siku ya harusi yake lakini
mwanamuziki huyo hakua akijua aliyekua akimzungushia viuno vya ngololo
ni nani.
0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)
Stay Informed With the Latest & Most Important News