AIBU..!! AUNT EZEKIEL ANA MIMBA NJE YA NDOA, YADAIWA INA MIEZI KADHAA ANGALIA HAPA

Admin Updates10 years ago6 Views


Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel akiwa viwanja na shosti yake, Wema Sepetu.

Madai mazito! Pamoja na kutumia nguvu kubwa
kukanusha kwa miezi kadhaa, bado staa wa sinema za Kibongo, Aunt
Ezekiel Grayson, anaendelea kugandwa na madai kwamba, amenasa mimba nje
ya ndoa, Ijumaa lina mkanda kamili.


Habari hizo zilishika kasi mithili ya moto wa kifuu baada ya Aunt
kunaswa Klabu ya New Maisha iliyopo Masaki jijini Dar, Jumapili
iliyopita akiwa ameshiba yaani kitumbo ndi huku akishindwa kukificha
baada ya kila kitu kuonekana waziwazi kwa macho yasiyohitaki miwani.


KIGAUNI CHAANIKA KILA KITU
Aunt, akiwa ukumbini
humo na mastaa wenzake waliohudhuria kwenye shoo ya msanii wa Bongo
Fleva aitwaye Mirrow anayesimamiwa na kampuni ya muigizaji, Wema Isaac
Sepetu na Meneja Petit Man, alitinga akiwa amevaa kigauni cha drafti
nyeupe na nyeusi ambacho kilionesha vilivyo tumbo lake.


WEMA ADAIWA KUMSINDIKIZA KLINIKI
Kwa mujibu wa
mpenda ubuyu wetu ambaye naye alikuwemo ukumbini humo, kwa kumtazama
Aunt anaonekana kuwa na ujauzito wa si chini ya miezi minne sasa na
kwamba Wema ambaye ni shosti wake anadaiwa kuwa huwa anamsindikiza
kliniki lakini staa huyo ameendelea kusisitiza kuwa hana.


UJAUZITO MIEZI MINNE

“Mimi najua muda mrefu na jinsi anavyoonekana kwa sasa hakuna ubishi
kwani ujauzito wake una kama miezi minne hivi,” kilisema chanzo chetu na
kuongeza:


 
Aunt Ezekiel akiwa na dansa wa ‘Diamond’, Mose Iyobo.


“Mwanamke mjamzito anajulikana kabisa. Hebu mcheki usoni
alivyobadilika. Yaani kawa mweupe wakati Aunt huwa ana rangi ya
chokuleti. Ukweli ni kwamba ana dalili zote za kubeba mimba.”


MAKE-UP YAMKATAA
Chanzo hicho kilizidi kuweka
wazi kwamba, siku hiyo, Aunt hakuwa amechangamka kama alivyozoeleka siku
zote na uso wake ulionekana kama mtu aliyechoka na hata ‘make-up’
aliyoweka haikuwa ikionekana vizuri.


NDUGU WAANZA MANENOMANENO
Habari zaidi zilidai
kwamba, baadhi ya ndugu na mawifi wa staa huyo wameanza kucharuka
wakidai kwamba Aunt atakuwa amepata ujauzito huo nje ya ndoa kwa kuwa
muda mrefu hajaonana na mumewe, Sunday Demonte anayedaiwa kuwa gerezani
huko Dubai.“Tangu mumewe apate matatizo Dubai hawajaonana hivyo Aunt
hawezi kusema ni ya mumewe,” kiliendelea kudai chanzo chetu.


VITABU VYA DINI
Baadhi
ya ndugu hao wametaka vitabu vya Dini ya Kiislam viweke wazi kama ni
sahihi kwa Aunt kubeba ujauzito nje ya ndoa kwani kwa upande wao
wanapinga kitendo hicho na kwamba ni udhalilishaji kwa ndugu yao ambaye
alifuata taratibu zote za kumuoa staa huyo.


Aunt Ezekiel wakati wa kufunga ndoa.


MNENGUAJI WA DIAMOND AHUSISHWA
Sosi huyo alidai
kwamba ujauzito wa Aunt unahusishwa na mnenguaji wa mwanamuziki wa Bongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Moze Iyobo ambaye kwa sasa
wamegandana kama kumbikumbi wakisemekana kuwa kwenye mahaba niue.


SHEHE ANASEMAJE?
Ili kuondoa utata huku
likijiridhisha kuwa Aunt anakaribia miaka miwili bila kukutana na
mumewe, gazeti hili lilizungumza na Shehe Kaima wa jijini Dar ambaye
analijua vizuri sakata la staa huyo ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Kwa kawaida mwanamke ambaye hajakutana na mumewe kwa miezi 6 au zaidi
baada ya ndoa, hupaswa kwenda mara moja Baraza Kuu la Waislam Tanzania
(Bakwata) kulalamika na hatimaye kudai talaka.


“Ikiwa mwanamke ameridhika na hali hiyo, naye akaamua kukaa kimya
huku akifanya mambo yake na kuanzisha uhusiano na wanaume wengine maana
yake amejitoa mwenyewe kwenye mamlaka ya mumewe, hivyo hapo kunakuwa
hakuna ndoa tena.”


AUNT ANASEMA?
Kama alivyojitetea siku ya
bethidei yake oktoba, mwaka huu baada ya kuvaa kigauni cha pinki
kilichoonesha kitumbo kikianza kuchomoza, katika tukio hilo la Jumapili
iliyopita, Aunt ameendelea kusisitiza kuwa ni aina ya magauni anayovaa
ndiyo yanayomuonesha na kitumbo lakini hana mimba.
“Sina huo ujauzito, labda ni kwa sababu ya aina ya magauni ninayovaa,” alisema Aunt kwa kifupi.


MIAKA MIWILI ILIYOPITA
Oktoba 18, 2012, Aunt
alifunga ndoa na Sunday ambapo mwigizaji huyo alibaki huku mumewe
akitimkia Dubai kabla ya baadaye kupata matatizo na kutupwa jela.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.