Ijumaa:
Wewe ni msanii lakini ni mke wa mtu, siku ukiwa hujaenda kwenye shughuli
zako za kisanii uwapo nyumbani huwa unafanya nini? Vanitha: Huwa
napenda kupikapika. Wewe ni mke wa mtu halafu ni sanii, je unapokuwa
nyumbani unapenda kumpikia chakula gani mumeo?
Vanitha: Nikiwa
nyumbani napenda kumpikia baby wangu chakula kizuri ambacho ni kipya.
Ijumaa: Je, pale unapokuwa faragha na mumeo unapenda kumtega kwa vivazi
gani?Vanitha: Ukweli huwa simtegi kwa mavazi, napenda kumtega kwa kukaa
mtupu kwani wakati huo huwa ni wake, kwa nini nimfichie mali zake?
Ijumaa: Ni upi ugonjwa wako uwapo faragha na huyo mumeo?
Vanitha: Napenda sana kumkumbatia na yeye anikumbatie. Kale kajoto
kanakotokea huku tukinong’onezana maneno matamu mimi nabaki
kusinziasinzia.
Ijumaa: Watu wanasema wanaume hawatabiriki kwa
kuchepuka, hivi siku ukimfumania mumeo utafanya nini?Vanitha: Naomba
Mungu isitokee kwani nahisi nitafanya tukio baya na kumuacha siwezi,
dah! Nahisi kutetemeka ukiniambia hivyo.
Vanitha Omary akipozi.
Ijumaa:
Mastaa wana skendo ya kuchukua waume za watu, wewe unamlindaje mumeo
asinaswe na wezi hao? Vanitha: Siwezi kusema nitamlinda kwani sijui mtu
anakuwa na nia gani na atakuwa amejipanga vipi ila nabaki kumuomba Mungu
amuepushe mume wangu na vishawishi.
Ijumaa: Kuna wanawake ambao
eti wanaona kuwapa waume zao mapenzi kinyume na maumbile ndiyo
kuwashika, wewe kwako likoje hili? Vanitha: Mungu aniepushie mbali kwani
ni jambo baya sana, sijawahi na sitowahi, nawaomba wanaofanya hivyo
kuacha kwani Mungu hapendi.
Ijumaa: Ni kitu gani kimewahi kukufurahisha katika maisha yako?
Vanitha: Nilifurahi sana siku niliyofunga ndoa na mume wangu kwani
tulipitia mikikimikiki mingi. Tumekaa kwenye uchumba kwa muda mrefu.
Ijumaa: Siku uliyohuzunika sana unaweza kuikumbuka?
Vanitha: Ni siku bibi yangu alipofariki, nakumbuka nilikuwa katika
wakati mgumu kwani yeye ndiye alikuwa mlezi wangu na nilikuwa na
ujauzito.
Ijumaa: Mbali na sanaa, ni kazi gani unaifanya?
Vanitha: Mimi ni mbunifu wa kupamba nyumba, nafanya kazi ya kuwadizainia
watu nyumba zao kwa mapambo mpaka muonekano mzima wa nyumba .